Registrar: registrar@judiciaryzanzibar.go.tz | Chief Court Administrator: cca@judiciaryzanzibar.go.tz

THE JUDICIARY OF ZANZIBAR

ZIARA YA MHESHIMIWA JAJI MKUU UNGUJA

HABARI

Mhe Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Khamis Ramadhan Abdalla amewataka wafanyakazi wa Mahkama kuwahudumikia Wananchi wanaokuja Mahkamani kupata huduma kwa kutumia lugha  nzuri na kuwafahamisha taratibu zote za  kimahkama kwa uwazi kabisa bila ya upendeleo wowote ule.

Hayo aliyasema  kwenye ziara zake za kuzitembelea Mahkama za Unguja  ili kujionea utendaji kazi wa Mahkama hizo na kusikiliza changamoto na kuzipatia ufumbuzi.

Aidha Mhe Jaji Mkuu amewaagiza Mahakimu dhamana wa Vituo hivyo  kutenga siku Maalumu kwa Ajili ya kusikiliza Malalamiko kwa wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.

Kwa upande wake Mrajis wa Mahkama Kuu Mhe Valentina A. Katema aliwapongeza wafanyakazi wa Mahkama hizo kwa  kazi nzuri wanazozifanya.

Aidha  Mhe Mrajis aliwataka wafanyakazi wa Mahkama  kuhakikisha kuwa hati za wito wa Mahkama  zinatolewa Mapema ili kuwafikia wahusika mapema.

Nao wafanyakazi wa Mahkama hizo wakieleza changamoto zinazowakabili walisema wanakabiliwa na uchache wa wafanyakazi kwenye vituo vyao vya kazi na   ufinyu wa nafasi katika Majengo ya Mahkama.

Kwa upande mwengine Mhe Jaji Mkuu wa Zanzibar amekabidhi Magari Mapya kwa Majaji  Watatu na Kadhi Mkuu akizigumza wakati wa makabidhiano hayo Mhe Jaji Mkuu aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwapatia Magari hayo ili kuondoa changamoto ya Usafiri kwa watumishi wa Mahkama.

Nae Mhe Kadhi Mkuu wa Zanzibar kwa niaba ya wahesimiwa Majaji alishukuru kwa kupatiwa Magari hayo na kuhakikisha kuwa watayatunza katika kipindi chote cha utumishi wao.                 

Unguja

High Court, Vuga
ZANZIBAR
Tel: +255 719 606 436
Email: info@judiciaryzanzibar.go.tz
Monday - Friday: 07:30am - 09:30pm
Saturday & Sunday: Closed

Pemba

High Court, Chake-Chake
ZANZIBAR
Tel: +255 719 606 436
Email: infopemba@judiciaryzanzibar.go.tz
Monday - Friday: 07:30am - 09:30pm
Saturday & Sunday: Closed