Skip to main content

New e-CMS system launching July 1, 2026 | Learn more

KAMATI YA BARAZA LA WAWAKILISHI YAPONGEZA MAHKAMA YA ZANZIBAR KWA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAKE

2026-10-29 Zanzibar Judiciary
Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya Kusimamia Afisi za Viongozi Wakuu wa Serikali, Mhe. Machano Othman Said, ameipongeza Mahkama ya Zanzibar kwa juhudi inazoendelea kuzichukua katika kutekeleza majukumu yake na kuboresha huduma za utoaji haki kwa wananchi.\r\nMhe. Machano ametoa pongezi hizo leo, tarehe 29 Oktoba, 2026, wakati Kamati hiyo ilipopokea na kujadili Ripoti ya Utekelezaji wa Majukumu ya Mahkama ya Zanzibar kwa kipindi cha Julai hadi Septemba, 2026.\r\nAmesema Kamati inatambua na kuthamini juhudi zinazofanywa na Mahkama ya Zanzibar katika kuimarisha ufanisi wa utendaji kazi, kuboresha miundombinu ya Mahkama pamoja na matumizi ya teknolojia katika kurahisisha huduma za utoaji haki.\r\nAidha, ameipongeza Mahkama kwa kuendelea kutekeleza maboresho mbalimbali yanayolenga kuongeza uwazi, uwajibikaji na kuimarisha imani ya wananchi kwa Mhimili wa Mahkama.\r\nMhe. Machano amesisitiza umuhimu wa kuendeleza juhudi hizo, huku akiwataka watendaji wa Mahkama kuendelea kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na uwajibikaji ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na haki kwa wakati.\r\nVilevile, amesema Kamati itaendelea kushirikiana na Mahkama ya Zanzibar katika kufuatilia utekelezaji wa majukumu yake, kutoa ushauri na kuhakikisha changamoto zinazojitokeza zinapatiwa ufumbuzi kwa lengo la kuimarisha sekta ya utoaji haki nchini.\r\nAmehitimisha kwa kuupongeza uongozi na watendaji wote wa Mahkama ya Zanzibar kwa kazi nzuri wanayoifanya, na kuwataka kuendeleza kasi ya maboresho ili kuhakikisha huduma za Mahkama zinakidhi matarajio ya wananchi.