JAJI MKUU WA ZANZIBAR AWATAKA MAJAJI WAKUU WA AFRIKA KUTUMIA MIKUTANO YA KIKANDA KUCHOCHEA MABORESHO YA MIFUMO YA UTOAJI HAKI
2026-10-06
Zanzibar Judiciary
Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla, amewataka Majaji Wakuu na viongozi wa Mahkama za kusini Mashariki mwa Afrika kuhakikisha kuwa mafunzo, uzoefu na maazimio yanayopatikana katika mikutano ya kikanda yanatafsiriwa kuwa hatua za vitendo zitakazochochea maboresho ya mifumo ya utoaji haki.rnMhe. Jaji Mkuu ameyasema hayo tarehe 6 Oktoba 2026, wakati akifunga h Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEACJF), uliofanyika katika Hoteli ya Verde, Zanzibar.rnAmesema mkutano huo umetoa fursa muhimu kwa Majaji Wakuu, Majaji, Mahakimu na viongozi wengine wa Mahakama kutoka nchi mbalimbali kubadilishana uzoefu, kujifunza mbinu bora na kuendeleza fikra za kisheria katika usimamizi na utoaji wa haki.rnAmesisitiza kuwa thamani halisi ya mijadala hiyo itaonekana pale ambapo maarifa, uzoefu na mawazo yaliyoshirikishwa yataweza kutafsiriwa kuwa maboresho yanayoonekana katika Mahakama za nchi wanachama. Ameongeza kuwa Mahakama zinapaswa kuendelea kujenga uwezo wa watendaji wake na kuandaa mipango ya utekelezaji inayozingatia mahitaji yanayobadilika ya Mahakama na jamii wanazozihudumia.rnAmesema hatua hizo zitasaidia kujenga Mahakama zinazowajibika zaidi, zenye ufanisi, zinazofikika kwa urahisi kwa wananchi na zenye uwezo wa kutoa haki kwa wakati na kwa ubora, huku zikilinda imani ya wananchi na kuimarisha utawala wa sheria.rnAidha, amewataka viongozi wa Mahakama kuhakikisha kuwa maazimio yaliyofikiwa katika mkutano huo yanatekelezwa katika taasisi zao, akisisitiza kuwa nguvu ya Mahakama haipo katika maamuzi yake pekee, bali pia katika uadilifu, uhuru, usawa, ufanisi na upatikanaji sawa wa haki kwa wote.rnKwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEACJF) ambaye pia ni Jaji Mkuu wa Kenya, Mhe. Martha Koome, amesema mkutano huo umewakumbusha washiriki kuwa Mahkama si sehemu za kusikiliza na kuamua mashauri pekee, bali ni taasisi zinazotegemea ushirikiano wa wataalamu wa kada mbalimbali ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.rnAidha, amesema uhuru wa Mahakama haupaswi kuishia katika uhuru wa kufanya maamuzi ndani ya vyumba vya Mahkama pekee, bali unapaswa pia kuambatana na uwezo wa taasisi hizo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.rnAmesisitiza kuwa Mahkama zinapaswa kuwa na rasilimali za kutosha zinazopatikana kwa wakati, pamoja na kuwa na uwezo wa kupanga vipaumbele na kusimamia rasilimali hizo kwa uwazi na uwajibikaji.rnMkutano huo uliwakutanisha Majaji Wakuu, Majaji, viongozi na watendaji wa Mahakama kutoka nchi mbalimbali za Kusini na Mashariki mwa Afrika kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kujadili mikakati ya kuimarisha mifumo ya utoaji haki katika ukanda huo. rn Masuala mbalimbali ya yalijadiliwa katika mkutano huo, yakiwemo uhuru wa kifedha wa Mahakama, Usuluhishi Mbadala wa Migogoro (ADR), matumizi ya Akili Bandia (AI), mageuzi ya kidijitali katika Mahakama, usimamizi wa Mahakama pamoja na uboreshaji wa mifumo ya utoaji haki.