Skip to main content

New e-CMS system launching July 1, 2026 | Learn more

WATENDAJI WAKUU WA MAHAKAMA ZA KUSINI NA MASHARIKI MWA AFRIKA WAKUTANA ZANZIBAR

2026-10-04 Zanzibar Judiciary
Watendaji Wakuu wa Mahakama kutoka nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika, kupitia Southern and Eastern Africa Judicial Administrators Association (SEAJAA), leo tarehe 4 Oktoba 2026, wamekutana Zanzibar kwa kikao kazi kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya utawala na uendeshaji wa Mahakama, pamoja na kubadilishana uzoefu kuhusu namna bora ya kuboresha utoaji wa huduma za haki kwa wananchi.\r\nKikao hicho, kilichofanyika katika Hoteli ya Verde, Zanzibar, kimetoa fursa kwa washiriki kujadili mikakati ya kuimarisha utendaji wa Mahakama, kuongeza ufanisi, kukuza matumizi ya teknolojia na ubunifu, pamoja na kuboresha mifumo ya utawala wa Mahakama kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma za haki kwa wananchi.\r\nSEAJAA inawakutanisha watendaji wa Mahakama kutoka nchi mbalimbali za Kusini na Mashariki mwa Afrika, zikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Botswana, Eswatini, Lesotho, Malawi, Mauritius, Mozambique, Namibia, Seychelles, Afrika Kusini, Zambia na Zimbabwe na Zanzibar kwa lengo la kuimarisha ushirikiano, kubadilishana uzoefu na kukuza ufanisi katika usimamizi na uendeshaji wa Mahakama.\r\nAidha, Watendaji Wakuu hao wanatarajiwa kushiriki katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEACJF), utakaofanyika Zanzibar kuanzia tarehe 5 hadi 9 Oktoba 2026.\r\nMkutano huo wa SEACJF unatarajiwa kuwakutanisha Majaji Wakuu na viongozi waandamizi wa Mahakama kutoka nchi wanachama kwa ajili ya kujadili masuala ya pamoja yanayohusu maendeleo ya sekta ya haki, mageuzi ya Mahakama na kuimarisha ushirikiano wa kimahakama katika ukanda wa Kusini na Mashariki mwa Afrika.