Skip to main content

New e-CMS system launching July 1, 2026 | Learn more

MAHKAMA YA ZANZIBAR YATOA MAFUNZO YA MFUMO WA UPIMAJI UTENDAJI KAZI KWA WATUMISHI WA MAHKAMA (PMS)

2026-09-30 Zanzibar Judiciary
Kaimu Mrajis wa Mahkama Kuu ya Zanzibar Mhe. Khamis Rashid Khamis, amesema kuwa Mfumo wa Upimaji Utendaji Kazi kwa watumishi ni nyenzo muhimu inayosaidia taasisi kuweka malengo ya kazi yaliyo wazi, kufuatilia utekelezaji wake, kupima matokeo yaliyopatikana na kubaini maeneo yanayohitaji kuboreshwa.\r\nMhe. Khamis ameeleza hayo wakati akifungua mafunzo ya Mfumo wa Upimaji Utendaji Kazi kwa watumishi Mahkama (PMS) yanayofanyika katika hoteli ya Madinat Al Bahri .\r\nAmesema matumizi ya Mfumo wa Upimaji Utendaji Kazi kwa watumishi PMS yataisaidia taasisi na watumishi kuelekeza juhudi zao katika malengo yaliyowekwa, pamoja na kupima kiwango cha utekelezaji wa malengo hayo kwa kutumia matokeo yanayoweza kupimika, kwani Mfumo wa PMS huunganisha malengo ya taasisi na matokeo yanayoweza kupimwa, hivyo kusaidia kuongeza uwazi, uwajibikaji na ulinganifu wa juhudi za watumishi na vipaumbele vya taasisi.\r\nAmesisitiza kuwa mfumo huo pia utaimarisha umakini, ulinganifu wa malengo na ushirikishwaji miongoni mwa watumishi, kwa kuwa kila mtumishi ataweza kuelewa malengo yanayopaswa kufikiwa na namna matokeo yake yanavyopimwa.\r\nAidha, ameeleza kuwa mafunzo hayo yana umuhimu mkubwa kwa Muhimili wa Mahkama na nchi kwa ujumla, kutokana na umuhimu wa kuwa na mfumo madhubuti wa kupanga, kufuatilia na kupima utendaji kazi ili kuhakikisha malengo ya taasisi yanafikiwa kwa ufanisi.\r\nMafunzo hayo yanayoendeshwa na kampuni ya “Epvate & Fortune International Consulting”, kutoka jijini Dar Es Salaam yanalenga kuwajengea washiriki uelewa na uwezo wa kutumia mfumo wa PMS katika usimamizi na ufuatiliaji wa utendaji kazi.\r\nMhe. Khamis amewataka washiriki kuyasikiliza na kuyazingatia kwa makini\r\n mafunzo hayo, na kuja kuyafanyia kazi yale yote mazuri waliyopatiwa, akieleza kuwa mfumo huo ni nyenzo muhimu katika kuweka na kupima utendaji wa watumishi kwa kuzingatia malengo na matokeo yaliyokusudiwa