Skip to main content

New e-CMS system launching July 1, 2026 | Learn more

MAHKAMA YA ZANZIBAR YATOA ELIMU KWA MASHEHA, WASAIDIZI WA SHERIA (PARALEGO) VIONGOZI WA DINI, MAKUNDI YA WANAWAKE NA VIJANA WA MKOA WA KUSINI UNGUJA

2026-09-26 Zanzibar Judiciary
Kaimu Mrajis wa Mahkama ya Zanzibar, Mhe. Khamis Rashid Khamis, amesema kuwa Masheha, Wasaidizi wa Sheria, Makundi ya Wanawake na Vijana na Viongozi wa Dini ni wadau muhimu wanaoshirikiana moja kwa moja na wananchi katika jamii, hivyo mafunzo yanayotolewa kwa makundi hayo yatasaidia kuwafikishia wananchi ujumbe na taarifa sahihi kuhusu mabadiliko na huduma zinazotolewa na Mahkama. \r\nMhe. Khamis ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya na washiriki wa mafunzo kuhusu Dhana ya Mabadiliko ya Mahkama yaliyohusisha Masheha, Wasaidizi wa Sheria, Makundi ya Wanawake na Vijana na Viongozi wa Dini wa Mkoa wa Kusini Unguja, akisisitiza umuhimu wa makundi hayo katika kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu huduma za Mahkama.\r\nSambamba na hilo, ameeleza kuwa dhana ya jinsia (gender) ina maana pana na haipaswi kuhusishwa na suala la mwanamke na mwanamme pekee, bali inahusisha pia namna jamii inavyowatambua, kuwahusisha na kuwapatia fursa watu katika mazingira mbalimbali. \r\nAidha, Mhe. Khamis amesisitiza kuwa maadili ni suala pana ambalo halihusu watendaji wa Mahakama pekee, bali ni muhimu jamii kwa ujumla kuelewa na kuzingatia misingi ya maadili inayohusiana na utoaji na upatikanaji wa haki. Amesema uelewa huo utasaidia kujenga mahusiano mazuri kati ya Mahkama, wadau na wananchi wanaotafuta huduma za haki.\r\nMhe. Khamis amewashukuru washiriki wa mafunzo ya Dhana ya Mabadiliko ya Mahkama kwa kuitikia wito na kushiriki katika mafunzo hayo, akieleza kuwa ushiriki wao ni muhimu katika kufanikisha juhudi za Mahkama za kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za haki.\r\n Amesema washiriki hao wanapaswa kutumia maarifa wanayoyapata katika mafunzo hayo kuwasaidia wananchi katika maeneo yao, hususan kwa kuwapatia taarifa sahihi na kuwaelekeza wananchi kwenye njia sahihi za kupata huduma za Mahkama.\r\nMafunzo kama hayo yameshafanyika kwa mikoa yote miwili ya Pemba ikiwa ni sehemu ya juhudi za Mahkama ya Zanzibar za kuimarisha ushirikiano na wadau katika kuboresha utoaji wa huduma za haki na kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu huduma, mifumo na mabadiliko yanayoendelea ndani ya Mahkama. Mabadiliko hayo yote yanafanyika chini ya Mradi wa Maboresho ya Mahkama (Zi-JUMP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (World Bank)