JAJI MKUU WA ZANZIBAR AKABIDHI VYETI VYA MAWAKILI NA MAVAKILI
2026-07-27
Zanzibar Judiciary
Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla, amewataka mawakili na mavakili kufanya kazi kwa uadilifu na kuepuka vitendo vinavyoweza kudhoofisha imani ya wananchi kwa mhimili wa Mahkama. \r\n\r\nMhe. Jaji Mkuu ameeleza hayo wakati akiwakabidhi vyeti mawakili na mavakili wapya, hafla iliyofanyika leo terehe 27 Julai, 2026 katika ukumbi wa Mahkama Kuu- Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja. Akisisitiza kuwa wananchi wengi hufika Mahkamani wakiwa na matumaini ya kupata haki, hivyo mawakili na mavakili wanapaswa kutanguliza maslahi ya haki badala ya maslahi binafsi.\r\n\r\nMhe. Jaji Mkuu aliongeza kuwa kuzingatia nidhamu katika kazi ni msingi wa taaluma ya sheria, huku akiwahimiza mawakili na mavakili hao kujiepusha na rushwa, ukiukaji wa siri za wateja na vitendo, vyovyote vinavyokiuka maadili ya kazi yao, na kuwataka kuwa mfano wa kuigwa katika jamii Sifa ya wakili haijengwi na ushindi wa kesi pekee, bali pia na uaminifu, nidhamu, heshima na uadilifu wake.\r\n\r\nAidha Mhe Jaji Mkuu amesema Kupokea cheti cha uwakili au uvakili si mwisho wa safari ya kujifunza, bali ni mwanzo wa jukumu kubwa la kuitumikia jamii kupitia taaluma ya sheria. Kuanzia leo, mtakuwa mabalozi wa haki, watetezi wa utawala wa sheria na walinzi wa misingi ya Katiba na haki za binadamu.\r\n\r\nMhe Jaji Mkuu alikumbusha kwamba taaluma ya uwakili na uvakili ni taaluma ya uadilifu. Jamii inawategemea kwa ushauri wa kisheria wenye weledi, uaminifu na uwajibikaji. wataaminiwa na watu wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali za kisheria, hivyo ni wajibu wao kuhakikisha wanatumia elimu na maarifa yao kwa manufaa ya wateja wao na taifa kwa ujumla.\r\n\r\nAkizungumza katika hafla hiyo, Naibu Mkuu wa Skuli ya Sheria Zanzibar, Nd. Msemo Mavare Semvua, amesema mawakili na mavakili wana wajibu mkubwa wa kulinda misingi ya haki na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kisheria na kuzingatia maadili ya taaluma yao, kuwa waadilifu, waaminifu na kuzingatia sheria katika utekelezaji wa majukumu yao.\r\n\r\nAidha, alisema lengo la mawakili ni kuisaidia Mahkama kufikia upatikanaji wa haki kwa kuhakikisha kesi zinaendeshwa kwa weledi na kwa kuzingatia misingi ya sheria. Pia amewataka mawakili na mavakili hao kushirikiana na Mahkama na wadau wengine wa sekta ya sheria katika kuimarisha utoaji wa haki nchini.\r\n\r\nJumla ya mawakili wapya 40 na mavakili 5 waekabidhiwa vyeti katika hafla iliyofanyika ikiwa ni hatua muhimu ya kuongeza nguvu kazi ya taaluma ya sheria na kuboresha utoaji wa huduma za haki nchini.