Skip to main content

New e-CMS system launching July 1, 2026 | Learn more

KADHI MKUU WA ZANZIBAR AWAKUMBUSHA WATUMISHI WA MAHKAMA YA KADHI KUENDELEA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

2026-06-30 Zanzibar Judiciary
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Mhe. Hassan Othman Ngwali amewakumbusha wafanyakazi wa Mahkama ya Kadhi kuendelea kusimamia maadili ya utumishi wa umma kwa kuepukana na vitendo vya rushwa, kwani huharibu taswira ya Mahkama na hupunguza imani ya wananchi katika mfumo wa utoaji haki. Kila mmoja anapaswa kuwa mfano wa uadilifu, uaminifu na uwajibikaji katika kutekeleza majukumu yake.rnAmeyasema hayo wakati wa ziara ya kuzitembelea Mahkama za Kadhi za Mkoa Kaskazini Unguja na Mkoa wa Mjini Magharibi kwa lengo kusikiliza changamoto.rnVilevile, Mhe. Kadhi Mkuu aliwahimiza kuongeza bidii katika kazi, kushirikiana kwa karibu na kujiandaa ipasavyo kwa matumizi ya mfumo mpya wa kielektroniki unaotarajiwa kuanza rasmi tarehe 1/07/2026. Alisema Mafanikio ya mfumo huo yatategemea utayari, nidhamu na ushirikiano wa kila mtumishi wa Mahkama.rnAidha alikuwakumbusha kuwa utoaji wa haki hauishii katika kutoa maamuzi sahihi pekee, bali pia unahitaji huduma zinazotolewa kwa haraka, kwa heshima na bila urasimu usio wa lazima. Alisema Wananchi wanaofika Mahkamani wanapaswa kuhudumiwa kwa weledi kwa wakati,rnKatika ziara hiyo Mhe. Kadhi Mkuu amembatana na viongozi mbali mbali akiwemo Naibu Kadhi Mkuu ,Mrajisi wa Mahkama ya kadhi na Watendaji wengine wa Mahkama.