JAJI MKUU WA ZANZIBAR NA UJUMBE WAKE WATEMBELEA UNIVERSTY SULTAN ZAINAL ABIDIN (UniSZA) TERENGGANU - MALAYSIA
2026-06-26
Zanzibar Judiciary
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdullah, akiambatana na ujumbe wake kutoka Mahkama ya Zanzibar, wamefanya ziara maalumu katika Universiti Sultan Zainal Abidin (UniSZA) mnamo tarehe 24 Juni 2026. Ziara hiyo imelenga kuboresha na kuimarisha utendaji wa Mahkama ya Kadhi Zanzibar kupitia ushirikiano na taasisi hiyo wa kukuza elimu ya kisheria kwa watendaji wa Mahkama za Zanzibar.\r\nKatika mapokezi rasmi yaliyofanywa na Naibu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Dr. Shukor bin Abd Razak, ujumbe waMahkama ya Zanzibar ulipata fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria, hususan nafasi ya UniSZA katika kutoa elimu ya sharia na mchango wake kwa mahkama za sharia nchini Malaysia.\r\nKikao cha majadiliano ya pamoja baina ya uongozi wa chuo na ujumbe wa Mahkama ya Zanzibar kilijadili masuala muhimu, ikiwemo fursa za masomo ya sharia ambazo Mahkama ya Zanzibar inaweza kunufaika nazo kupitia chuo hicho.\r\nKatika neno lake la shukurani, Mheshimiwa Jaji Mkuu wa Zanzibar alieleza kufurahishwa kwake na mapokezi mazuri na utayari wa UniSZA kushirikiana na Mahkama ya Zanzibar katika sekta ya sharia. Aidha, alikabidhi zawadi rasmi kwa chuo hicho zikiwemo:\r\n1. Sheria ya Mahkama ya Kadhi Nam. 8/2023\r\n2. Kanuni za Mahkama za Kadhi (Mwenendo na Tataratibu), 2024\r\n3. Kanuni za Ndoa na Talaka kwa Mahkama ya Kadhi Zanzibar\r\n4. Kanuni za Rufaa kutoka Mahkama ya Kadhi ya Rufaa kwenda Mahkama Kuu.\r\nZiara hii imefungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa kimataifa kielimu na kisheria kati ya Zanzibar na Malaysia, na inatarajiwa kuleta manufaa makubwa katika kuboresha mifumo ya sharia na utendaji wa Mahkama ya Kadhi Zanzibar