Skip to main content

New e-CMS system launching July 1, 2026 | Learn more

MHE. LYIMO ATOA UFAFANUZI JUU YA USIKILIZWAJI WA MASHAURI YA MAHAKAMA YA RUFANI

2026-06-15 Zanzibar Judiciary
Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Dyness Redson Lyimo amesema jumla ya mashauri 49 yanatarijiwa kusikilizwa na kutolewa uamauzi katika Kikao cha Mahakama Rufani ya Tanzania kilichoanza Rasmi leo tarehe 15 June hadi 10 July 2026 katika Jengo la Mahakama Kuu Tunguu. Ambapo kati ya mashauri hayo, mashauri 20 ni ya jinai, 27 ya madai pia maombi ya madai moja na jinai moja.rnrnMhe. Lyimo ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari akisisitiza kuwa lengo la ujio huo ni kusikiliza kesi zote ambazo zimekatiwa rufaa ili kuhakikisha wananchi wanapatiwa haki zao kwa mujibu sheria.rnrnAidha, amefahamisha kuwa kikao hicho kinaongozwa na jopo la Majaji watatu wakioongozwa na Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Barke Mbaraka Sehel.rnrnMhe. Lyimo ametoa wito kwa wananchi waliokata rufaa kutoa ushirikiano wa kutosha na kusikiliza kesi zao ili kuhakikisha haki inapatikana kwa wahusika wa mashauri hayo.