JAJI IBRAHIM AFUNGUA KIKAO CHA KAMATI YA KUSUKUMA MASHAURI MBELE
2026-06-10
Zanzibar Judiciary
Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Ibrahim Mzee Ibrahim amesema Kuanzishwa kwa Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Mashauri ni hatua kubwa katika safari ya kuibadilisha Mahkama kutoka mfumo wa kawaida wa karatasi kwenda katika mfumo wa kisasa wa kidijitali. rnAmeyasema hayo wakati akifungua kikao cha Kamati Kuu ya Kusukuma mbele mashauri ya haki jinai na haki madai kilichofanyika katika Ukumbi wa Mahkama Kuu Tunguu .rnAidha alisema Mfumo huu utawezesha usajili wa mashauri, ufuatiliaji wa hatua mbalimbali za Mashauri, upangaji wa tarehe za usikilizaji, utunzaji wa kumbukumbu za mashauri na upatikanaji wa taarifa kwa ufanisi zaidirnAlisema Kikao hicho kinatoa fursa ya kujadili kwa kina kiwango cha utayari wa Mahkama katika kuanza rasmi matumizi ya mfumo . Ni muhimu kujiridhisha kuwa miundombinu ya TEHAMA ipo tayari, watumishi wamepatiwa mafunzo ya kutosha, vifaa vinavyohitajika vinapatikana na taratibu zote za kiutendaji zimekamilika kabla ya kuanza kutumika kwa mfumo huo.rnMhe Jaji Ibrahim alisema kikao kitatoa nafasi ya kujadili changamoto zilizobakia na kuweka mikakati ya pamoja ya kuhakikisha kuwa tarehe itakayopangwa kwa ndio uzinduzi na kuanza rasmi kwa matumizi ya mfumo inafikiwa kwa mafanikio. Mafanikio ya mfumo huu yanategemea ushirikiano, wa wadau, nidhamu ya kazi na utayari wa kila mtumishi wa Mahkama kuendana na mabadiliko ya teknolojiarnKwa upande wake Mwakilishi wa ujenzi mfumo Ndugu Khatib Pandu Buyu ameeleza kuwa watumiaji wakubwa wa mfumo huo ni wananchi ambapo wamebaba asilimia 70% jambo ambalo limeweza kuleta tija pindi utakapoanza kutumika kwa mfumo huo. rnKwa upande wao wadau wa Mahkama wameupongeza uongozi wa Mahkama kwa hatua nzuri waliyoichukua kwa kuanzisha mfumo huo wa usikilizwaji wa mashauri kwa njia ya kidigitali ambapo wameahidi kutoa mashirikiano mkubwa kwa Mahkama ili kuweza kufanikisha mfumo huo.