Skip to main content

New e-CMS system launching February 1, 2026 | Learn more

MAHKAMA YA ZANZIBAR YAPOKEA GARI MPYA 18 KUBORESHA UTENDAJI KAZI

2026-05-05 Zanzibar Judiciary
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla leo amepokea gari 18 mpya zilizotolewa na Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Maboresho ya Mahkama ili kuimarisha utendaji kazi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za haki kwa wananchi.\r\nAkizungumza katika hafla ya makabidhiano ya gari hizo, Jaji Mkuu alieleza kuwa ujio wa gari hizo itarahisisha utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya Mahkama. \r\nMhe Jaji Mkuu alitoa shukrani za dhati kwa Benki ya Dunia kwa ushirikiano wao endelevu na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika juhudi za kuimarisha sekta ya haki. Mradi huu wa maboresho ya Mahkama ni kielelezo cha dhamira ya pamoja ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, kwa wakati na kwa ufanisi\r\nAidha, Mhe Jaji Mkuu amezishukuru Serikali zote mbili, serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa msaada wao mkubwa uliowezesha Mahkama ya Zanzibar kupata ufadhili wa mradi wa Maboresho ya Mahkma unaofadhiliwa na Benki ya Dunia\r\nAlisisitiza kuwa magari hayo yataongeza ufanisi wa kazi za Mahkama na kusaidia watendaji kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi, ndani na nje ya maeneo yao ya kazi.\r\nKwa upande wake mwakilishi kutoka banki ya dunia bibi Donna Andrews amesisitiza kuwa lengo mradi huo ni kusaidia kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wananchi kwa kuboresha miundombinu na huduma za Mahakama. Ameeleza kuwa magari haya yatasaidia kuongeza ufanisi wa utendaji kazi, hususan katika kuwafikia wananchi waliopo maeneo ya mbali, na kuimarisha usimamizi wa shughuli za kimahakama\r\nAidha, amebainisha kuwa Benki ya Dunia itaendelea kushirikiana na Zanzibar katika miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha mifumo ya utoaji haki, kwa kuzingatia uwazi, uwajibikaji na matumizi bora ya rasilimali.\r\nNae, Mratibu wa mradi wa Maboresho ya Mahkama Mhe. Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim alieleza kuwa gari hizo zitatumika kikamilifu katika kukuza utendaji, ufanisi na uwajibikaji wa watumishi wa Mahkama. Aliongeza kuwa rasilimali hizo zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta matokeo chanya kwa Taasisi na jamii kwa ujumla.