Skip to main content

New e-CMS system launching February 1, 2026 | Learn more

JAJI IBRAHIM AFUNGUA RASMI MAFUNZO YA NJIA MBADALA YA UTATUZI WA MIGOGORA (ADR)

2026-04-05 Zanzibar Judiciary
Jaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar Mhe, Ibrahim Mzee Ibrahim amesema matumizi ya njia mbadala za utatuzi wa migogoro (ADR) yatakuwa suluhisho muhimu katika kupunguza mlundikano wa mashauri mahakamani na kuongeza ufanisi katika utoaji wa haki.rnAkifungua mafunzo ya siku tano yanayowakutanisha wadau wa Mahkama wakiwemo mawakili wa Serikali na wa kujitegemea, pamoja na Mavakili yanayofanyika Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja, katika hotel ya Visitor Inn Mhe. Jaji Ibrahim amesema kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kuleta mageuzi ya mfumo wa utoaji haki Zanzibar.rnAidha alisema ADR inatoa fursa kwa wahusika wa mgogoro kushiriki kikamilifu katika kutafuta suluhisho la migogoro wao kwa njia ya mazungumzo, usuluhishi na maridhiano. Njia hii si tu inapunguza gharama na muda, na kulinda mahusiano kati ya wahusika.rnAmesema kuwa tayari njia ya usuluhishi imeanza kutumika kwa upande wa Mahkama ya Kadhi Zanzibar na inatarajiwa kuanza kutumika pia katika mahkama za kawaida. Amefafanua kuwa matumizi ya njia ya usuluhishi yatasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano wa kesi pamoja na kuharakisha upatikanaji wa haki kwa wananchi.rnAidha, ameeleza kuwa jamii inawategemea sana wadau wa mahkama katika kutatua migogoro wanyokabiliana nayo, hivyo ni muhimu kushiriki kikamilifu katika mafunzo hayo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.rnKwa upande wake, muwezeshaji wa mafunzo hayo Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Abdalla Halfan Gonzi, amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo washiriki kupitia kubadilishana ujuzi na uzoefu katika utekelezaji wa usikilizaji wa mashauri kwa njia ya usuluhishi.rnAmefafanua kuwa mafunzo hayo yanalenga kuimarisha uelewa wa wadau wa Mahkama kuhusu umuhimu na matumizi sahihi ya njia mbadala za usuluhishi katika kutatua migogoro ya kisheria.