Skip to main content

New e-CMS system launching February 1, 2026 | Learn more

UFUNGUZI WA MAONESHO YA MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA ZANZIBAR 2026

2026-02-06 Zanzibar Judiciary
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mhe. Rashid Hadid Rashid amewataka wananchi kuitumia vyema fursa ya maonesho ya Wiki ya Sheria Zanzibar kwa kuwauliza wataalamu wa sheria maswali yenye tija kwao, ili kupata uelewa mpana wa masuala ya kisheria yanayowahusu na haki zao za msingi. \r\n\r\nMhe. Rashid ameyasema hayo wakati akifungua maonesho ya Wiki ya Sheria Zanzibar kwa mwaka 2026 yanayofanyika Gombani ya Kale-Pemba, huku akimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwiynyi kwa maono yake makubwa ya kutaka kuiona Zanzibar inakwenda sambamba na maendeleo ya kiteknolojia, hususan katika uendeshaji wa shughuli za Mahkama. \r\n\r\nAmesisitiza kuwa katika zama za sasa za utandawazi, matumizi ya mifumo ya kielektroniki hayakwepeki, hivyo wadau wa sheria wanapaswa kwenda sambamba na mabadiliko ya kiteknolojia.\r\n\r\nAmeeleza kwamba matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika uendeshaji wa mashauri yatachangia kwa kiasi kikubwa kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wakati kwa wananchi, akisisitiza kuwa haki iliyocheleweshwa ni sawa na haki iliyonyimwa hivyo ni vyema kutumia mifumo ya kielektroniki ili haki isichelewe kupatikana.\r\n\r\nPia, Mhe. Rashid amempongeza Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla kwa jitihada zake za kuanzisha na kuimarisha mifumo ya kidijitali katika Mahkama, akieleza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kuongeza ufanisi, uwazi na kuimarisha imani ya wananchi kwa mhimili wa Mahkama.\r\n\r\nNae, Jaji Mkaazi Pemba, Mhe. Salum Hassan Bakari, amewaomba wadau wa sheria kuendelea kupigania haki za wananchi kwa misingi ya haki, usawa na utawala wa sheria. Vilevile, kuwasisistiza wananchi kutojichukulia sheria mikononi mwao, bali kutumia njia halali za kisheria kwa kufika Mahkamani kutafuta haki zao.\r\n\r\nAmesema Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Zanzibar yanafanyika kwa lengo la kutoa elimu ya sheria kwa wananchi, kuimarisha uelewa wa haki na wajibu wa kila mmoja, pamoja na kuonesha maboresho mbalimbali yanayofanyika katika sekta ya haki nchini.\r\nVilevile, amemshukuru Mhe. Rashid pamoja na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo kwa mchango wao mkubwa katika kuhakikisha maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanafanyika katika hali ya usalama, amani na utulivu.\r\n\r\nMaonesho ya Wiki ya Sheria yanafanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Sheria Zanzibar kwa mwaka 2026.