JAJI MKUU AFUNGUA MKUTANO MKUU WA ZAJOA
2026-01-17
Zanzibar Judiciary
JAJI MKUU WA ZANZIBAR AFUNGUA MKUTANO MKUU WA ZAJOA\r\n\r\nJaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadha Abdalla amewataka Majaji, Makadhi na Mahakimu kuongeza kasi ya usikilizaji wa mashauri na kuyatolea maamuzi kwa haraka ili kujenga imani kwa wananchi. \r\nWakati akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Mahakimu na Majaji Zanzibar (ZAJOA) uliyofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA) Maruhubi Mkoa wa Mjini Magharibi, amesema Serikali imejitahidi kutatua maombi yote ya msingi yaliyoombwa na Mahkama ikiwemo maslahi ya watumishi, hivyo ni wajibu wa watumishi wa Mahkama kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na uweledi ili kutimiza malengo yaliyowekwa.\r\n\r\nAidha, ameeleza kuwa Mahkama itaendelea kusimamia maadili kwa watendaji wake kwa lengo la kulinda utu na kusimamia maslahi mapana ya jamii na kuitaka ZAJOA kufanya tafiti mbalimbali za kisheria pamoja na kutoa mafunzo kwa jamii ili wananchi waelewe uwepo wa chama hicho na malengo yake. Sambamba na kuwaasa kuwa wabunifu katika utendaji wa majukumu yao.\r\n\r\nNae, Rais wa ZAJOA Jaji wa Mhkama Kuu ya Zanzibar Mhe. Salma Ali Hassan amesema lengo la mkutano huo ni kutoa elimu mbalimbali kwa wajumbe na wanachi kwa ujumla juu ya masuala ya mifuko ya jamii, masuala ya kibenki na elimu ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ambapo wawasilishaji wa mada kutoka ZSSF, PBZ na ZAECA wamealikwa kwa ajili ya kutoa elimu hiyo.\r\n\r\nAmeeleza kuwa, mkutano huo pia utakua na jukumu la kuchagua viongozi wapya watakaoongoza kwa awamu nyengine na kuahidi kuwa watachagua viongozi makini na wenye uwezo kwa maslahi mapana ya chama na wananchi kwa ujumla.