Skip to main content

New e-CMS system launching February 1, 2026 | Learn more

JAJI MKUU AFUNGUA MAJARIBIO YA MFUMO WA KUSIKILIZA MASHAURI KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI K

2025-12-27 Zanzibar Judiciary
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla amesema mfumo wa usikilizaji wa Mashauri kwa njia ya Kielektroniki utapelekea kumalizika kwa haraka Mashauri Mahkamani pamoja na kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wananchi.\r\n\r\nAmesyasema hayo wakati akifungua majaribia ya Mfumo wa usikilizaji wa Mashauri wa njia ya Kielektroniki (Electronic Case Management System- eCMS) yanayofanyika katika hotel ya Madinat Bahr mbweni\r\n\r\nAidha Mhe Jaji Mkuu amesema mfumo wa kielektroniki ni dhamira ya dhati ya Mahkama ya Zanzibar ya kuimarisha utoaji wa haki kwa wakati, kwa uwazi, na kwa ufanisi zaidi. Mfumo huu ni sehemu ya jitihada za Mahkama kuendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia katika utoaji wa huduma za Mahkama.\r\nVile vile Mhe. Jaji Mkuu amesema kupitia mfumo huu Utamuwezesha mwananchi akiwa sehemu yoyote kuweza kufungua au kusikiliza mwenendo shauri lake na kupata taarifa muhimu zinazohusiana na Mashauri kwa haraka kwa kutumia simu yake ya kiganjani ya aina yoyote ile, mwananchi ataweza kupokea ujumbe wa taarifa zake za kesi bila kufika Mahkamani. \r\n\r\n“Majaribio haya ni hatua muhimu ya kubaini changamoto, na kupata maoni ya wadau wote ili kuuboresha mfumo huu kabla ya kutumika rasmi katika Mahkama zetu. Ni matarajio yangu kuwa Majaji, Mahakimu, Makadhi, Mawakili na wadau wote wa Mahkama mtatoa ushirikiano wa karibu ili kuhakikisha mfumo huu unafanya kazi kwa ufanisi kama unaokusudiwa” alisema Mhe. Jaji Mkuu.\r\n\r\nMajaribio hayo yamewajumuisha watendaji wa Mahkama, Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, , Afisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mafunzo, Polisi, Afisi ya usajili wa Matukio ya Kijamii, Afisi ya vitambulisho vya Taifa, Mawakili,