Skip to main content

New e-CMS system launching February 1, 2026 | Learn more

KADHI MKUU WA ZANZIBAR AWAAPISHA WASULUHISHI

2025-12-12 Zanzibar Judiciary
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Mhe. Sheikh Hassan Othman Ngwali amewataka wasuluhishi kua waaminifu na kufanya kazi zao kwa kuzingatia haki bila ya kuegemea upande wowote kwa sababu ya undugu, urafiki na tamaa za kidunia.\r\nAmeyasema hayo wakati wa hafla fupi ya kuwaapishi wasuluhishi wawili wa mahkama ya Kadhi iliyofanyika ofisini kwake Tunguu Wilaya ya Kati Unguja.\r\n\r\nAidha, amefahamisha kua wasuluhishi wanatakiwa kusikiliza pande zote kwa subra na hekima bila ya kukurupuka katika kutoa suluhu huku wakielewa kua maneno ya watu yanaweza kua na hisia tofauti, kejeli au hata uongo ndani yake, lakini hayo yote yasiwavunje moyo na kuwakatisha tamaa katika kufikia suluhu.\r\n\r\nAmeeleza kua, wasuluhishi wanatakiwa watoe suluhu kwa kuzingatia mafunzo ya Mtume (S.A.W) kwani yeye alikua mkarimu, msamehevu, na daima alitafuta njia ya kutuliza nafsi na kuokoa ndoa na familia.\r\n \r\nMhe. Kadhi Mkuu amesisitiza ya kwamba wasuluhishi watoe suluhu zitakazodumu na sio za muda mfupi zitakazowafanya wenye mgogoro kurudi tena katika mgogoro wao punde tu baada ya usuluhishi kwani suluhu ya kweli hujengwa kwa ukweli, ushauri na ufuatliaji.\r\n\r\nAmehitimisha kwa kuwanasihi na kuwapongeza wasuluhishi waliyoapishwa pamoja na kuwanasihi wananchi kwa ujumla ya kwamba wamtegemee Allah na kumuomba msaada wake kwa sala na dua pindi wanapojikuta katika hali ngumu au migogoro migumu sambamba na kutafuta ushauri kwa wenye hekima.