JAJI MKUU AONGOZA KIKAO CHA KUJADILI KANUNI ZA MAHKAMA KUU KUTOKA MAHKAMA YA KADHI YA RUFAA
2025-12-10
Zanzibar Judiciary
JAJI MKUU WA ZANZIBAR AONGOZA KIKAO KAZI CHA KUPITIA KANUNI MWENENDO WA MAHKAMA KUU KUTOKA MAHKAMA KADHI YA RUFAA \r\nJaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla, amesema kutungwa kwa kanuni za uendeshaji wa mwenendo wa Mahkama Kuu kutoka Mahkama ya Kadhi wa Rufaa zina lengo la kuboresha na kurahisisha mwenendo wa mashauri yanayokatiwa rufaa kutoka Mahkama ya Rufaa ya Kadhi, sambamba na kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wakati.\r\nMhe. Jaji Mkuu ameyasema hayo wakati akifungua kikao kazi cha kupitia wa kanuni za uendeshaji za Mahkama Kuu kutoka Mahkama ya Kadhi wa Rufaa ikilichofanyika katika hoteli ya Madinat Al Bahar iliyopo Mbweni Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.\r\nAkizungumza na washiriki wa kikao hicho wakiwemo Majaji wa Mahkama Kuu, Makadhi na Mawakili Mhe. Jaji Mkuu alisema kuwa kanuni hizo mpya zinatoa mwongozo wa wazi kuhusu namna ya kuwasilisha rufaa, nyaraka zinazopaswa kuwasilishwa, muda wa kuyawasilisha, pamoja na wajibu wa kila upande katika usikilizwaji wa mashauri hayo.\r\nAidha, ameeleza kua uwepo wa kanuni hizo ni hatua muhimu katika kujenga mfumo wa haki unaoeleweka, wenye ufanisi na unaozingatia misingi ya sheria na maadili ya utoaji haki na zitapunguza ucheleweshaji wa mashauri na kuongeza uwazi katika uendeshaji wa rufaa.\r\nAidha, alisisitiza kuwa utekelezaji wa kanuni hizo utahitaji mashirikiano ya karibu kati ya wadau wote wa sheria ili kuhakikisha mazingira ya utoaji haki yanakuwa thabiti na yenye kuaminika, pamoja na kuwataka mawakili kutilia umuhimu kuhudhiuria vikao kazi pindi wanapoalikwa kwa maslahi makubwa ya nchi.\r\nKanuni hizo zimetungwa kwa misingi ya mamlaka aliyopewa Jaji Mkuu wa Zanzibar chini ya kifungu cha 19 cha Sheria ya Mahkama Kuu, Na. 2 ya 1985 na zitatumika mara tu baada ya kukamilika na kutangazwa katika gazeti rasmi la serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.