Skip to main content

New e-CMS system launching February 1, 2026 | Learn more

NAIBU KADHI AFUNGUA MAFUNZO YA USULUHISHI

2025-12-01 Zanzibar Judiciary
Naibu kadhi Mkuu wa Zanzibar Mhe. Othman Ame Choum amesema Sula la Usuluhishi katika Mahkama za Kadhi utasaidia Mahkama katika kutatua baadhi ya migogoro inayoletwa Mahkamani \r\n\r\nAmeyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya usuluhishi kwa makadhi na wasuluhishi yaliyofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip uwanja wa ndege Zanzabar \r\nAlisema mafunzo hayo yana umuhimu mkubwa katika kuimarisha uwezo wa Makadhi na Wasuluhishi ili waweze kusimamia vyema misingi ya usuluhishi kulingana na sheria, maadili na taratibu sahihi za Kiislamu na kimahkama.\r\n\r\n“Ni imani yangu kuwa mafunzo haya yatachangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha utoaji wa haki, kupunguza mlundikano wa mashauri, na kuongeza imani ya wananchi katika Mahkama ya Kadhi kama taasisi ya haki, amani na utatuzi wa migogoro kwa njia rafiki na yenye staha.” Alisema Mhe. Othman.\r\n\r\nAidha alisema Dunia ya sasa inashuhudia mageuzi makubwa katika utoaji wa huduma za haki. Mfumo wa usuluhishi na mbinu nyingine za “Alternative Dispute Resolution (ADR) zimeendelea kuthibitisha kuwa ni njia bora, na haraka, zisizo na kuchukuwa muda mkubwa na kuhifadhi mahusiano ya wahusika.\r\nMafunzo hayo ya siku tano yanaendeshwa chini ya Mradi wa Maboresho ya Mahkama unaofadhiliwa na benki ya Dunia na kuwashirikisha Makadhi na Wasuluhishi na kuendeshwa na wakufunzi kutoka chuo cha Uongozi wa Mahkama Lushoto.