JAJI IBRAHIM AFUNGU MAFUNZO KWA MAVAKIL
2025-11-29
Zanzibar Judiciary
Jaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar Mhe Ibrahim Mzee Ibrahim amewataka Mavakili kuwa wazalendo, wakweli na waaminifu Katika utendaji wa kazi zao ili Jamii ijenge imani nao wakati wanapowawakilisha Mahkamani.\r\n\r\nAkizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo mavakili na wanafunzi kutoka skuli ya sheria Zanzibar yaliyofanyika katika hoteli ya Madina tul Bahar mbweni.\r\nAidha alisema uvakili ni taaluma ya heshima, taaluma ya uadilifu, na ni taaluma inayohitaji maandalizi makini na ufuasi wa kanuni, hivyo ni vyema kufanya kazi zao kwa weledi ili kuboresha utendaji kazi kwa maslahi ya wananchi na ustawi wa mfumo wa haki.\r\n\r\nVile vile alieleza kuwa Mafunzo haya yameandaliwa kwa lengo la kuongeza uelewa wa kina juu ya taratibu za kisheria, mwenendo wa mashauri, na kanuni za kiutendaji katika mfumo wa Mahkama za Zanzibar. Kwa dunia ya sasa ambapo taratibu za sheria zinabadilika kwa kasi, ni muhimu kwa kila vakili kuhakikisha anajiridhisha na kiwango cha uelewa wake.\r\n\r\nKwa upande wake Naibu Mrajis wa Mahkama Kuu ya Zanzibar Mhe. Faraji Shomari Juma amesema Mafunzo haya ni hatua muhimu katika safari ya kuimarisha utendaji wa wanasheria nchini na kuboresha utoaji wa haki.\r\n\r\nMafunzo hayo yameendeshwa chini ya Mradi wa Maboresho ya Mahkama unaofadhiliwa na benk ya Dunia kutoa Mafunzo kwa wadau wa Mahkama ili kuleta mashirikiano mazuri kati yao na Jamii kwa Ujumla.