Skip to main content

New e-CMS system launching February 1, 2026 | Learn more

JAJI MKUU ATEMBELEA KAMBI YA UJENZI WA MFUMO WA USIMAMIZI WA MASHAURI KWA NJIA YA KIELETRONIKI

2025-10-23 Zanzibar Judiciary
JAJI MKUU ATEMBELEA KAMBI YA UJENZI WA MFUMO WA USIMAMIZI WA MASHAURI KWA NJIA YA KIELETRONIKI.\r\n\r\nJaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla amesema kumalizika kwa mfumo wa usimamizi wa Mashauri kwa njia ya kieletroniki kutaleta mageuzi makubwa ya kiutendaji katika upokeaji na usikilizaji wa Mashauri yanayowasilishwa Mahkamani.\r\nameyasema hayo leo katika ziara ya kutembelea kambi ya wataalamu wa ujenzi wa mfumo wa usimamizi wa mashauri Mahkamani (e Case Management System) huko Mkoani Pemba.\r\nAidha Mhe. Jaji Mkuu alisema kuwa Mfumo huo ni chombo muhimu kitakachobadilisha kabisa namna ya Mahkma inavyosimamia mashauri katika Mahkama, ambapo Mashauri yatapangwa, kufuatiliwa na kusikilizwa kwa uwazi na ufanisi mkubwa. Na zaidi ya yote wananchi watapata huduma za Mahkama kwa njia rahisi, za haraka na zisizo na urasimu.\r\n\r\nMhe. Jaji Mkuu aliwapongeza wataalam wa kambi hiyo kwa kazi nzuri sana inayoendela kufanywa kwa kujitolea kwao, ubunifu na kwa moyo wa kizalendo kwani wanachokifanya katika kazi hiyo ni mchango mkubwa katika historia ya haki nchini.\r\n“endeleeni na kazi kwa weledi, kwa uadilifu, na kwa uzalendo. Kumbukeni kuwa mfumo huu si wa TEHAMA pekee, bali ni wa haki za wananchi wetu. Kila mstari wa “code” mnaoandika, kila ramani ya mfumo mnaopanga, ni hatua moja mbele katika kujenga Mahkama yenye ufanisi, uwazi, na inayoendana na mahitaji ya kizazi cha kidigitali.”\r\n\r\nKatika ziara hiyo Mhe. Jaji Mkuu amepata fursa ya kuona vipengele vya mfumo ambavyo ujenzi wake umekamilika ikiwa ni pamoja na namna ya kujisajili katika mfumo kwa watumiaji wa ndani ya Mahkama na watumiaje wa nje, ufunguaji wa mashauri kielektroniki, upokewaji na upangaji kwa Mahkama ya kawaida pamoja na Mahkama ya Kadhi.\r\nAnae kwa upande wake Kiongozi wa kambi hiyo Mr. Khatib Pandu Buyu amemueleza Mhe, Jaji Mkuu kua ujenzi wa mfumo kwa sasa umefikia asilimia 43.80% ambapo kwa mujibu wa mpango kazi wa ujenzi asilimia iliyopaswa kua imefikiwa kwa sasa ni 45.80% kiongozi huyo ameeleza kua asilimia 2.20% zilizopungua zimetokana na mapendekezo ya majaribia pili yaliyofanyika kwa watumiaji wa mfumo. \r\nKatika ziara hiyo i Mhe. Jaji Mkuu aliongozana na Jaji wa Mahkama Kuu Mhe. Khadija Shamte Mzee, Mtendaji Mkuu wa Mahkama ya Zanzibar Mhe Kai B. Mbaruk, Naibu Mrajis wa Mahkama wa Kuu Mhe. Chausiku Kuya, pamoja na watendaji wengine wa Mahkam.\r\nKambi hiyo inaundwa na wataalamu kutoka Mahkama ya Zanzibar kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Mahakama ya Tanzania.