Skip to main content

New e-CMS system launching February 1, 2026 | Learn more

JAJI MKUU AFANYA ZIARA YA KIKAZI, AWATAKA WATENDAJI WA MAHKAMA KUWA WABUNIFU

2025-10-21 Zanzibar Judiciary
JAJI MKUU AFANYA ZIARA YA KIKAZI, AWATAKA WATENDAJI WA MAHKAMA KUWA WABUNIFU\r\n\r\nJaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla, amewataka watendaji wa Mahkama kuongeza ubunifu ili kuongeza kasi ya utendaji wa kazi zao na kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wananchi. \r\nAkizungumza na wafanyakazi wa Mahkama ya Mkoa wa Kusini Unguja iliyopo Tunguu amesema kulingana na kasi ya maendeleo inayofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwemo ujenzi wa majengo ya kisasa ya Mahkama ni vyema wafanyakazi kuwa wabunifu ili kuongeza kasi ya utendaji na kuleta mabadiliko yenye mafanikio kwa wananchi kama ilivyokusudiwa. \r\n\r\nMhe. Jaji Mkuu amefahamisha kuwa lengo la kuzungumza na wafanyakazi katika maeneo yao ya kazi ni kuhakikisha mafanikio yanapatikana pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili kwa wakati. Sambamba na hayo, amewataka Mahakimu kuzitatua kesi kwa wakati na kuhakikisha wananchi wanapatiwa haki zao kama inavyostahiki. \r\n\r\nNae Hakimu dhamana wa Mkoa wa Kusini Unguja, Mhe. Mohamed Amour Haji ameishukuru Serikali kwa kuwajengea Majengo ya kisasa yenye huduma zote za kimahkama na kuahidi kuwa watayatumia majengo hayo kufanya kazi kwa ufanisi ili kuleta mabadiliko chanya na mafanikio makubwa katika kutoa haki.\r\nKwa upande wao, watumishi wa Mahkama hiyo waliushukuru uongozi wa Mahkama pamoja na kumshukuru binafsi Mhe, Jaji Mkuu kwa uongozi wake makini unaojali watumishi wake pamoja kuzingatia haki za wananchi na wameahidi kuendeleza nidhamu, ushirikiano na uwajibikaji katika kazi zao.