JAJI MKUU ATEMBELEA MAHKAMA YA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA
2025-10-15
Zanzibar Judiciary
Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mheshimiwa Khamis Ramadhan Abdalla, amesema uwajibikaji, maadili na mapambano dhidi ya rushwa katika mfumo wa utoaji haki ni jambo la wajibu kwa kila mtumishi wa Mahkama. Ameyasema hayo katika ziara yake ya kikazi ya kuwatembelea watendaji wa Mahkama ya Mkoa wa Kaskazini Unguja iliyopo kiongele\r\n\r\nAkizungumza na watumishi hao, Jaji Mkuu amesema kuwa Mahkama ni nguzo muhimu katika kuhakikisha haki inapatikana kwa wakati na kwa usawa, hivyo ni wajibu wa kila mtumishi wa Mahkama kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu, uwazi na ufanisi mkubwa na kuachana na vitendo vinavyokiuka maadili ya kimahkama ikiwemo rushwa na kujihusisha na siasa.\r\n\r\nAidha, Jaji Mkuu alisisitiza umuhimu wa kuongeza bidii katika utendaji kazi wa kila siku, ikiwemo usikilizwaji wa mashauri kwa wakati ili kupunguza mrundiko wa kesi unaosababisha ucheleweshaji wa haki huku akiwaahidi watumishi hao kuwatatulia kero zinazowakabili kwa wakati ili kuongeza ufanisi wa kazi.\r\n\r\nKwa upande wao, watumishi wa Mahkama hiyo walimshukuru Jaji Mkuu kwa uongozi wake makini na kwa kufika kuwasikiliza moja kwa moja, wakiahidi kuendeleza nidhamu, ushirikiano na uwajibikaji katika kazi zao.