Skip to main content

New e-CMS system launching February 1, 2026 | Learn more

JAJI IBRAHIM AFUNGUA MAFUNZO YA KUKUSANYA NA KUWASILISHA USHAHID WA KIELEKTRONIKI MAHKAMANI KWA WADAU WA MAHKAMA.

2025-10-13 Zanzibar Judiciary
Jaji wa Mahkma Kuu ya Zanzibar Mhe. Ibrahim Mzee Ibrahim amema katika zama hizi za maendeleo ya teknolojia, matumizi ya ushahidi wa kielektroniki yamekuwa sehemu muhimu ya mfumo wa utoaji wa haki, hiyo ni wajibu wa wadau wa sekta ya sheria n kuhakikisha wana uelewa wa kina juu ya namna bora ya kukusanya, kuhifadhi, na kutumia ushahidi kielektroniki kwa mujibu wa sheria.\r\n\r\nJaji Ibrahim ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku tatu yanayohusiana na ushahidi wa kielektroniki na teknolojia zinazoibuka (AI) kwa waendesha Mashtaka Mahkamani yenye lengo la kuimarisha utendaji wa shughuli za Mahkama za kila siku, Mafunzo hayo yanayofanyaki katika hoteli ya Zanzibar Ocean View iliyopo Kilimani Mjini Zanzibar. \r\nAidha, Mhe. Jaji Ibrahim ameeleza kua ushahidi wa kielektroniki na teknolojia kwa wakati uliopo hauwezi kuepukika, hivyo ni jukumu la wadau wa sekta Sheria kujipanga na kujiweka imara kwa kujifunza namna bora ya kukusanya na kuwasilisha ushahidi wa kielekroniki mbele ya Mahkama. \r\nVile Vile alisema Mafunzo haya pia ni sehemu ya mpango mpana wa maboresho ya Mahkama za Zanzibar, unaolenga kuongeza ufanisi, uwazi na matumizi ya teknolojia katika utendaji kazi wake. Mahkama imeweka msukumo mkubwa katika kuimarisha uwezo wa watendaji wake, kuboresha miundombinu ya kidigitali, na kuhimiza utamaduni wa kushirikiana kati ya taasisi zote za haki.\r\n\r\nNae Mkufunzi wa Mafunzo Jaji wa Mahkama Kuu ya Tanzania kanda Tabora Mhe. Dkt Adam Mambi ameeleza kua malengo ya mafunzo hayo ni kuwawezesha washiriki kuelewa jinsi ya kushughulikia ushahidi wa kielektroniki kuanzia eneo la tukio hadi Mahkamani pamoja na kuelewa sheria na kanuni zinazosimamia ushahidi wa kielektroniki. \r\nMafunzo hayo ya siku tatu yanajumuisha wadau mbalimbali wa sekta Sheri kutoka Serikalini na binafsi wakiwemo Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Zanzibar (ZAECA), Jeshi la polisi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Zanzibar (DPP), Chama cha Mawakili Zanzibar, Mahkama za Wilaya, Mikoa na Mahkama Kuu Zanzibar, Kitengo cha upelelezi, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Zanzibar.