KADHI MKUU ATEMBELEA KAMBI YA KUTENGENEZAJI WA MIFUMO YA KIELEKTRONIKI YA USIMAMIZI WA MASHAURI

2025-10-10
Zanzibar Judiciary
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Mhe. Hassan Othman Ngwali ametembelea kambi ya utengenezaji Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Mashauri (eCMS) iliyopo Mkoani Pemba.\r\n\r\nKiongozi wa kambi hiyo Mr. Khatib Buyu amemueleza Mhe. Hassan Namna kazi hiyo inavyoendelea, pamoja na hatua iliyofikiwa hadi sasa, na kuahidi kumalizika kwake ndani ya muda uliopangwa na kwa ufanisi mkubwa, ambapo ndani ya wiki hii kambi itafanya UAT ya pili tokea zoezi hilo lianze mapema mwezi August mwaka huu.\r\n\r\nKwa upande wake Mhe. Kadhi Mkuu ameitumia fursa hiyo kuwapongeza wanakambi kwa kazi nzuri na kubwa pamoja na uzalendo wao wa kujitoa na kukubali kua mbali na familia zao kwa maslahi ya taifa, na amewanasihi kuendelea kua hivyo na bila ya kuonesha kuchoka bali waongeze juhudi ya kuhakikisha mfumo unakamilika ndani ya muda uliopangwa na kwa ufanisi mkubwa.