Registrar: registrar@judiciaryzanzibar.go.tz | Chief Court Administrator: cca@judiciaryzanzibar.go.tz

THE JUDICIARY ZANZIBAR

JAJI MKUU AWAAPISHA MAKADHI WAPYA

Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla amewataka MAKADHI wapya  kuwa  waadilifu wakati wanapotekeleza Majukumu  yao kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi   ili kulinda heshima na hadhi ya Mahkama kwa ujumla.

Alimeyasema hayo wakati wa  sherehe za kuwaapisha Makadhi wapya wanne zulizofanyika katika ukumbi wa Mahkama kuu Tunguu.

Aidha, Mhe. Jaji Mkuu wa Zanzibar amewaasa Makadhi hao wapya kuzingatia maadili ya Viongozi wa Umma  na Maadili ya maofisa wa Mahakama ikiwa ni pamoja na kujaza fomu za tamko la Mali na madeni kwa mujibu wa sheria.

Aliwakumbusha Makadhi hao wapya kuwa  wao  ni Viongozi wa umma na kwa hivyo hawapasi kuvunja Maadili yanayohusiana na kazi yao.

Vilevile , Mhe Jaji Mkuu  aliwakumbusha  Makadhi hao kuwa, Mahakama ipo kwenye maboresho hivyo inawapasa  na wao waendane na   kasi ya Maboresho hayo kwa kusikiliza na kuyatolea maamuzi kwa haraka Mashauri yote yatakayoletwa  mbele yao.

kwa upande wake Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman aliwataka Makadhi hao wapya kusimamia  viapo kwa kutenda haki na kuzingatia uafilifu wakati wa  kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Kwa upande wake, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Mhe Hassan Othman Ngwali akitoa salamu zake kwenye ghafla hiyo amawataka Makadhi hao kuwa makini sana wakati wanapowasikiliza wadawa wanaofika mbele yao kwa kuwapa haki sawa ili kuondoa malalamiko yasiyokuwa na uladhima . Makadhi  walioapishwa katika HAFLA hiyo ni  Sheikh Abdul-azizi Saleh Juma, Sheikh Hemed Saleh Abdalla, Sheikh Ali Juma Machano na Sheikh Taraik Abdalla Kassim

Unguja

High Court, Vuga
ZANZIBAR
Tel: +255 719 606 436
Email: info@judiciaryzanzibar.go.tz
Monday - Friday: 07:30am - 09:30pm
Saturday & Sunday: Closed

Pemba

High Court, Chake-Chake
ZANZIBAR
Tel: +255 719 606 436
Email: infopemba@judiciaryzanzibar.go.tz
Monday - Friday: 07:30am - 09:30pm
Saturday & Sunday: Closed