Registrar: registrar@judiciaryzanzibar.go.tz | Chief Court Administrator: cca@judiciaryzanzibar.go.tz

THE JUDICIARY ZANZIBAR

ZIARA YA MHE JAJI MKUU PEMBA

 Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Khamis Ramadhan Abdalla amewataka wafanyakazi wa Mahkama Pemba kuhakikisha kuwa wanayafanyia kazi kwa haraka mashauri yanayofikishwa Mahkamani ili kujenga Imani kwa wananchi pale wanapofikisha mashauri yao Mahkamani.

Ameyasema hayo katika  ziara yake ya kuzitembelea Mahkama za Pemba na chou cha Mafunzo ili kujionea utendaja kazi wa watendaji wa Mahkama hizo na  kusikiliza changamoto zinazowakabili ili kuzipatia  ufumbuzi.

Amesema kwa sasa Wananchi wengi wamepoteza Imani na Mahkama kufuatia kucheleweshwa kusikilizwa kwa Kasi zao zinapofikishwa Mahakamani

Aidha Mhe Jaji Mkuu amewataka wanafunzi walikuwepo kwenye vvyo vya mafunzo kukata rufaa ikiwa hawakuridhika na adhabu waliopewa na Mahkama husika ili Mahkama za juu ziweze kuzifanyia kazi rufaa zao, pia Mhe Jaji Mkuu aliwaahidi wanafunzi hao kuwa uongozi wa Mahkama utahakikisha kuwa mienendo ya kesi inapatikana mapema ili kuweza kukata rufaa.

Akizungumza mara baada ya kutambulishwa kwa watendaji wa Mahkama Pemba Mrajis wa Mahkama Kuu Zanzibar Mhe Valentina A. Katema amewasisitiza wafanyakazi kuongeza bidi katika usikilizaji wa Mashauri ili kuondoa usumbufu kwa wananchi na kuondoa Mrundikano wa kesi Mahkamani.

 

Kwa upande wake Naibu Mrajis wa Mahkama Kuu Pemba Mhe Faraji Juma Shomari alimewataka wafanyakazi wa Mahkama pemba kutoa  mashirikiano kwa  Mrajis huyo ili kufanikisha kazi zake kwa ufanisi.

Nao wafanyakazi wa Mahkama hizo wameeleza changamoto mbali mbali zinazowakabili ikiwemo uhaba wa vitendea kazi,

Katika ziara hiyo iliyofanyika katika Mkoa wa kusini Pemba jumla ya Mahkama Tatu  zilitembelewa ikiwa ni Pamoja na Mahkama Ardhi, Mahkama ya wilaya Mkoani na Mahkama ya Mwazo kengeja na chou cha  mafunzo kengeja.

 

Unguja

High Court, Vuga
ZANZIBAR
Tel: +255 719 606 436
Email: info@judiciaryzanzibar.go.tz
Monday - Friday: 07:30am - 09:30pm
Saturday & Sunday: Closed

Pemba

High Court, Chake-Chake
ZANZIBAR
Tel: +255 719 606 436
Email: infopemba@judiciaryzanzibar.go.tz
Monday - Friday: 07:30am - 09:30pm
Saturday & Sunday: Closed