KIKAO CHA MRAJIS NA WAANDISHI WA HABARI
Jumla ya mashauri mapya 5089 yamepokelewa katika mahkama mbali mbali za unguja na pemba katika
kipindi cha miezi mitatu kuanzia jully mpaka september 2022.
hayo yalisemwa na mrajisi wa mahkama kuu zanzibar mh valentina a. katema alipokuwa akizungumza na
wandishi wa habari afisini kwake mahkama kuu tunguu wakati akitoa ripoti ya utendaji wa kazi wa
mahkama kwa kipindi cha miezi mitatu akitoa ufafanuzi wa mashauri hayo amesema katika mahkama kuu
kumepokelewa mashauri mapya 164 ambayo kati ya hayo 42 ni ya jinai, rufaa za jinai 17 na maombi ya
jinai 39.
na kwa upande wa madai kumepokelewa mashauri 18, rufaa za madai 17 na maombi ya madai 31.
kwa upande wa divisheni ya mahkama ya biashara kumepokelewa shauri moja na divisheni ya mahkama
ya kazi kumepokelewa mashauri 8.
kwa upande wa kesi za udhalilishaji jumla ya mashauri mapya 127 yamepokelewa.
na kwa upande wa mashauri ya madawa ya kulevya jumla ya mashauri mapya 51 yalipokelewa mahkamani
na kwa upande wa mahkama ya ardhi jumla ya mashauri mapya 57 yalipokelewa kwa kipindi cha miezi
mitatu.
na kwa upande wa makosa ya usalama barabarani jumla ya mashauri 3859 yalipokelewa na kati ya hayo
mashauri 3822 yamekutwa na hatia na kutozwa faini na mashauri 37 yamesalia mahkamani.
kwa upande wa mahkama ya kadhi jumla ya mashauri mapya 597 yalipokelewa katika mahkama hiyo kwa
kipindi cha miezi mitatu na kati ya hayo mashauri 538 yamemalizika.
aidha mrajis wa mahkama kuu mh valentina amesema mahkama imefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi
milioni mia moja sabini na moja laki mbili sitini na tatu na shilingi hamsini na sita.
akitoa wito kwa jamii mh mrajis ameitaka jamii kuisaidia mahkama kwa mashahidi kufika mahkamani
kutoa ushahidi ili kuharakisha kumalizika kwa mashauri yaliyokuwepo mahkamani. aidha alisema
mahkama iko tayari kushirikiana na wadau wake wote ili kuifanya mahkama kuwa ni kimbilio sahihi kwa
wanaotafuta haki.