Registrar: registrar@judiciaryzanzibar.go.tz | Chief Court Administrator: cca@judiciaryzanzibar.go.tz
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla amewataka Majaji, Mahakimu na Makadhi kufanya kazi zao kwa uweledi na kujiamini katika kutoa haki bila ya kuingiliwa katika utoaji wa maamuzi yao.
Ameyasema hayo Leo katika Mkutano wa 17 wa Chama Cha Majaji na Mahakimu Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi.
Amesema Mahakama ni chombo huru ambacho kinafanya kazi zake bila ya kusimamiwa na taasisi nyengine yeyote. Pia amewashauri Majaji na Mahakimu pamoja na Makadhi kujiamini na kuhakikisha wanatoa maamuzi ya mashauri kwa wakati ili kupunguza malalamiko ya wananchi kuhusu ucheleweshaji wa kesi.
Aidha Jaji Mkuu ameishukuru serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Dkt Hussein Ali Mwinyi kwa kuwapatia vitendea kazi na kuwaomba wanachama hao kuvitunza na kutumia vitendea kazi katika kuandikia hukumu za mashauri pamoja na kuhakikisha mienendo ya kesi inapatikana kwa wakati.
Kwa upande wake Jaji wa Mahkama Kuu Mhe. Salma Ali Hassan ambae pia ni Raisi wa Chama hicho amesema kukutana kwao kwa pamoja ni fursa adhimu ambayo inapelekea kutatua changamoto zinazowakumba katika kazi zao za kila siku za utoaji hukumu kwa wananchi pamoja na kuelezea mafanikio yanayo patikana kutoka katika Jumuia hiyo.
Jumuia ya Majaji ,Mahakimu na Makadhi (ZAJOA) imeanzishwa mwaka 2007 ambapo imewakutanisha Majaji Mahakimu na Makadhi wa Mahkama ya Zanzibar.
High Court, Vuga
ZANZIBAR
Tel: +255 719 606 436
Email: info@judiciaryzanzibar.go.tz
Monday - Friday: 07:30am - 09:30pm
Saturday & Sunday: Closed
High Court, Chake-Chake
ZANZIBAR
Tel: +255 719 606 436
Email: infopemba@judiciaryzanzibar.go.tz
Monday - Friday: 07:30am - 09:30pm
Saturday & Sunday: Closed