Registrar: registrar@judiciaryzanzibar.go.tz | Chief Court Administrator: cca@judiciaryzanzibar.go.tz
Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla amewataka Mahakimu na Makadhi kuzitunza na kuzithamini vitendea kazi walivyopatiwa ili kuhakikisha kazi zinafanyika kwa ufanisi na kwa haraka zaidi.
Ameyasema hayo katika hafla ya kuwakabidhi vitendea kazi komputa mpakato(Laptop) kwa Mahakimu pamoja na Makadhi ikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa wanaachana na matumizi ya karatasi na badala yake kwenda na wakati kwa kutumia komputa mpakato na kuweza kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu.
Aidha Jaji Mkuu ameishukuru Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuweza kuwapatia fedha kwa ajili ya ununuzi vitendea kazi hivyo ikiwemo laptop, desktop na scanner. Lengo ikiwa ni kuboresha huduma zinazotolewa na Mahkama.
Nae Mrajis wa Mahkama Kuu Zanzibar Mhe. Valentina Andrew katema amewataka Mahakimu pamoja na Makadhi kutumia vitendea kazi hivyo kwa kutoa nakala za hukumu kwa wakati pamoja na kuendelea na matumizi ya mfumo wa tehama.
Kwa upande wao baadhi ya Mahakimu wameupongeza uongozi wa Mahkama kwa kwenda na teknolojia ya kisasa na kuachana na matumizi ya karatasi na kuahidi kufanya kazi kwa bidii na kwa uweledi ili kuweza kutoa haki kwa wakati na kujenga imani kwa Jamii.
Jumla ya computer 115 zimenunuliwa na kugaiwa kwa Mahakimu, Makadhi na watendaji wengine wa Mahkama Unguja na Pemba.
High Court, Vuga
ZANZIBAR
Tel: +255 719 606 436
Email: info@judiciaryzanzibar.go.tz
Monday - Friday: 07:30am - 09:30pm
Saturday & Sunday: Closed
High Court, Chake-Chake
ZANZIBAR
Tel: +255 719 606 436
Email: infopemba@judiciaryzanzibar.go.tz
Monday - Friday: 07:30am - 09:30pm
Saturday & Sunday: Closed