Registrar: registrar@judiciaryzanzibar.go.tz | Chief Court Administrator: cca@judiciaryzanzibar.go.tz

THE JUDICIARY OF ZANZIBAR

KIKAO CHA MAHKMA NA MAWAKILI WA SERIKALI NA WAKUJITEGEMEA.

Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla amewataka Mawakili wa Serikali pamoja  wa kujitegemea  kuwa na mashirikiano   Mahkama ili kuweza kutatua changamoto   wanazokabiliana nazo kwa  lengo la  kuhakikisha kuwa haki kwa wananchi zinapatikana bila upendeleo wa aina yeyote. 

    Ameyasema hayo leo wakati alipofungua kikao cha pamoja baina ya  Mawakili wa Serikali , Mawakili wa kujitegemea na Mahkama  huko Afisi kwake  Tunguu kikiwa na lengo la kujadiliana jinsi gani ya kuweza kuzitatua changamoto zinazowakabili na kujipanga katika mwaka 2024 ili kuona Wananchi wanapata haki zao kwa wakati.

      Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka ndugu Mwanamkaa Abdurahman  ameushukuru Uongozi wa Mahkama kwa kuandaa kikao hicho cha kuwakusanya pamoja wadau mbali mbali wa Mahkama kwa lengo la kutafuta njia ya kuweza kuisaidia jamii katika upatikanaji wa haki

       Nae Raisi wa Chama cha Mawakili  Zanzibar ndugu Masoud Lukazibwa amesema ipo haja kubwa ya kufanya vikao hivyo mara kwa mara ili kuondoa changamoto zinazowakabili na kutafuta njia mbadala ya kutatua changamoto  hizo.

       

 Kikao hicho kimewashirikisha Mahakimu, Makadhi Afisi ya Mwanasheria Mkuu, Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Pamoja na  Mawakili wa kujitegemea zanzibar. 

 

Unguja

High Court, Vuga
ZANZIBAR
Tel: +255 719 606 436
Email: info@judiciaryzanzibar.go.tz
Monday - Friday: 07:30am - 09:30pm
Saturday & Sunday: Closed

Pemba

High Court, Chake-Chake
ZANZIBAR
Tel: +255 719 606 436
Email: infopemba@judiciaryzanzibar.go.tz
Monday - Friday: 07:30am - 09:30pm
Saturday & Sunday: Closed