A PHP Error was encountered

Severity: Warning

Message: fopen(/var/cpanel/php/sessions/ea-php80/ci_session0996f3e99236e50b2a69346aa995aac72dbf639f): Failed to open stream: No space left on device

Filename: drivers/Session_files_driver.php

Line Number: 176

Backtrace:

File: /home/court/public_html/web/application/controllers/Posts.php
Line: 23
Function: __construct

File: /home/court/public_html/web/index.php
Line: 315
Function: require_once

A PHP Error was encountered

Severity: Warning

Message: session_start(): Failed to read session data: user (path: /var/cpanel/php/sessions/ea-php80)

Filename: Session/Session.php

Line Number: 143

Backtrace:

File: /home/court/public_html/web/application/controllers/Posts.php
Line: 23
Function: __construct

File: /home/court/public_html/web/index.php
Line: 315
Function: require_once

The Judiciary of Zanzibar

Registrar: registrar@judiciaryzanzibar.go.tz | Chief Court Administrator: cca@judiciaryzanzibar.go.tz

THE JUDICIARY OF ZANZIBAR

ZIARA YA TUME YA UTUMISHI WA MAHKAMA TANZANIA

Sekretariet ya Tume ya Utumishi wa Mahakama Zanzibar imefungua ukurasa mpya wa ushirikiano baada ya kukukutana na Sekretariet ya Tume ya Utumishi wa Mahkama ya Tanzania kwa lengo la kufahamiana na kubadilishana uzoefu wa kazi katika masuala ya utoaji haki.

Akizungumza  katika mkutano huo Mtendaji Mkuu wa Mahkama Zanzibar Kai B Mbaruk alimpongeza katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahkama Tanzania kwa kuzaa wazo la kuja kuitembelea  sekretariet ya Tume ya Utumishi wa Mahkama kwani jambo hilo ni la muhimu sana na litaleta mafanikio kwa pande zote Mbili.

Akifungua Mkutano baina ya Tume hizo mbili katibu wa Tume ya Utumishi ya Mahkama Tanzania ambae pia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania  Prof. Elisante Ole Gabriel amewataka watumishi wa Sekretariet hizo zote mbili kujadiliana kwa kina kuhusu mambo manne ambayo ni muundo wa Tume hizo, mambo hayo ni Pamoja na  nidhamu na maadili, matumizi ya Teknolojia(Tehama) katika utoaji haki na kuongeza imani ya wananchi kwa muhimili wa Mahakama.=

Alisema ni muhimu wajumbe hao kujadili kuhusu muundo wa Tume kwa pande zote mbili za Muungano ili kuona mchango wake katika masuala ya utoaji haki.  Aliongeza kuwa japokuwa kuna tofauti ya muundo wa Tume kati ya Tanzania bara na Zanzibar lakini haki ni jambo linalogusa watu wote.

Katibu huyo wa Tume pia amewataka wajumbe wa Mkutano huo kujadiliana namna ya kushirikiana katika matumizi ya Teknolojia ya habari na mawasiliano kwenye  shughuli za utoaji wa haki.Alisema Mahakama ya Tanzania hivi sasa imepiga hatua kubwa kwenye matumizi hayo ambapo inayo mifumo mbalimbali ya kurahisisha kazi ya utoaji haki.

Aidha Prof. Elisante Ole Gabriel alitoa wito kwa watumishi wa Sekretaet zote mbili za Tume ya Utumishi wa Mahkama kuwa na nidhamu ya hali ya juu wanapotekeleza majukumu yao ili kujenga taswira chanya ya Mahakama kwa wadau wake.

”Nidhamu ni jambo la msingi na muhimu kwa watumishi wa Mahkama kwani bila nidhamu kwa watumishi wa Muhimili huo ni vigumu kwa wananchi kuwa na imani na Mahkama, pia inarahisisha mnyororo wa utoaji haki”, alisema Katibu wa Tume.

Aliwataka watumishi hao wa Tume kulinda taswira nzuri ya Mhimili wa Mahkama iliyojengeka ili wananchi wawe na imani zaidi na mhimili huo ambapo alisema tathmini iliyofanyika hivi karibuni inaonesha kuwa kiwango cha imani ya wananchi kwa Mahkama kimeongezeka kutoka asilimia 65 mwaka 2015 na kufikia asilimia 88 mwaka huu wa 2023.

Kwa upande wake, Katibu wa Tume hiyo kwa upande wa Zanzibar ambaye pia ni Naibu Mrajis Mhe. Salum Hassan Bakari alisema Mkutano huo baina ya Tume hizo mbili ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi aambapo alizitaka taasisi za Serikali kwa pande zote mbili za Muungano kushirikiana katika kuwahudumia wananchi.

Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahkama  pamoja na watumishi wa Sekretariet walikuwa katika ziara ya siku mbili visiwani humo iliyoanza tarehe 11/09/2023 hadi Septemba 12, mwaka 2023.

Unguja

High Court, Vuga
ZANZIBAR
Tel: +255 719 606 436
Email: info@judiciaryzanzibar.go.tz
Monday - Friday: 07:30am - 09:30pm
Saturday & Sunday: Closed

Pemba

High Court, Chake-Chake
ZANZIBAR
Tel: +255 719 606 436
Email: infopemba@judiciaryzanzibar.go.tz
Monday - Friday: 07:30am - 09:30pm
Saturday & Sunday: Closed