Registrar: registrar@judiciaryzanzibar.go.tz | Chief Court Administrator: cca@judiciaryzanzibar.go.tz

THE JUDICIARY ZANZIBAR

MKUTANO ULIOSHIRIKISHA WADAU WA SHERIA

Kaimu jaji Mkuu wa zanzibar mhe Khamis Ramadhan amewashauri Majaji , Mahakimu kutumia lugha ya kiswahili wanapoandika mienendo ya kesi na wanapotoa hukumu zao ili kuwarahisishia wananchi ambayo hawafahamu lugha ya kiengereza. Aliyasema hayo ofisini kwake tunguu kwenye kikao cha wadau wa mfumo wa haki jinai. Aidha Mhe khamis alisema lengo la kikao hicho ni kuleta maboresho kwenye mfumo wa haki jina ili kuondosha malalamiko kwa jamii na kurejesha iman kwa wananchi juu ya mfumo wa haki jinai Zanzibar. Wakichangia kwenye kikao hicho wadau hao walisema kuwa bado kuna tatizo la kuchelewa kupatikana kwa nakala ya miendendo ya kesi pamoja na hukumu hali ambayo inachelewesha utaratibu mzima wa kukata rufaaa pale ambapo mwananchi hakuridhika na maamuzi husika. Aidha walisema kuwa kuna tatizo la ucheleweshaji wa kuanza kwa kesi kunakosababishwa na afisi ya mkurugenzi wa mashtaka kwa kisingizio cha kumuaanda shahidi wakati wa kesi hali ambayo inawafanya wapoteze muda mwingi mahakamani. Kikao hicho kiliwajumuisha wadau wa mfumo wa haki jinai zanzibar wakiwemo Majaji, mahakimu Makadhi, jeshi la polisi, Afisi ya mkurugenzi wa Mashtaka, mawakili, mavakili, pamoja na ZAECA.

Unguja

High Court, Vuga
ZANZIBAR
Tel: +255 719 606 436
Email: info@judiciaryzanzibar.go.tz
Monday - Friday: 07:30am - 09:30pm
Saturday & Sunday: Closed

Pemba

High Court, Chake-Chake
ZANZIBAR
Tel: +255 719 606 436
Email: infopemba@judiciaryzanzibar.go.tz
Monday - Friday: 07:30am - 09:30pm
Saturday & Sunday: Closed