icon-rss-large

Email: info@judiciaryzanzibar.go.tz |  | Web Mail |

  • zanzibar high court

  • zanzibar high court

  • zanzibar high court

  • zanzibar high court

  • zanzibar high court

  • zanzibar high court

  • zanzibar high court

 

current news

Published on /May 18, 2015, 1:25 pm/By Mr.Balu.


JAJI MKUU AFUNGUA MAHKAMA YA BIASHARA

Jaji Mkuu wa Zanzibar akikata utepe wa kuashiria kufunguzi wa Mahkama ya biashara Zanzibar. Jaji Mkuu wa Zanzibar amesema kuanzishwa kwa Mahkama ya Biashara kutatoa unafuu mkubwa wa utatuzi wa migogoro inayohusiana na mambo ya biashara na kupatiwa uamuzi ndani ya muda mfupi,ambapo mashauri ya aina hiyo yalikuwa yanachukua muda mrefu katika Mahkama za Kawaida. Aidha Mhe. Jaji Mkuu wa Zanzibar alisema Sheria ya Mahkama ya Biashara no.9 ya mwaka 2013 imejaribu kuepuka vipingamizi vinavyopatikana katika sheria ya Mwenendo wa Madai ya sura ya 8 ya Sheria za Zanzibar, ambapo ina masharti Magumu na sio Rafiki kwa wafanyabiashara, mashirika,mabenki na Makampuni Vile vile Mhe. Jaji Mkuu wa Zanzibar aliwatanabahisha wananchi kwamba kufunguliwa kwa Mahkama ya Biashara hakuondoi uwezo wa Mahkama nyengine kuendelea kusikiliza migogoro ya aina hiyo, Mahkama ya Biashara ni Mbadala wa Mahkama nyingine kwa wadawa ambao wanataka migogoro yao itatuliwe kwa njia ya haraka kwani Sheria inataka shauri lolote litakalo fikishwa mbele ya Mahkama ya Biashara kutolewa uamuzi ndani ya Miezi kumi hadi kumi na mbili. Nae Jaji wa Mahkama ya Biashara Mhe. Rabia Hussen Mohammed alisema atahakikisha mashauri yote yatakayofunguliwa katika ya Mahkama ya Biashara yatasikilizwa na kutolewa uamuzi wa viwango kwa muda mfupi na kuhakikisha haki inapatikana katika mashauri ya kibiashara kwa wote. Sherehe hiyo lifanyika katika jengo la Mahkama ya Biashara lililopo vuga na kuhudhuriwa na Majiji wa Mahkama kuu, Naibu Katibu Mkuu wa Wira ya Katiba na Sheria na Wadau wengine.

current news

Published on /May 7, 2015, 1:10 pm/By Mr. Balu.


JAJI MKUU WA ZANZIBAR AWAAPISHA MAHAKIMU WALIOPANDA DARAJA

Jaji Mkuu wa Zanzibar akimuapisha Mhe. Nassem Fakih Mfaume kuwa Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo. Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu amewaapisha Mahakimu wapya kumi na sita waliopanda daraja, kutoka ngazi moja kwenda nyengine akizungumza katika sherehe hiyo ya kuwaapisha Mahakimu hao Mhe,Jaji mkuu aliwataka kufanya kazi zao kwa uadilifu na kufuata kanuni na sheria zilizopo. Vile vile Mhe,Jaji Mkuu aliwataka Mahakimu hao kukumbuka viapo vyao wakati wote kwani vinawataka kufanya kazi bila ya chuki wala upendeleo, pia aliipongeza tume ya utumishi wa Makhama kwa kazi nzuri ya Kuchagua Mahakimu hao. Sherehe hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Mahakama Kuu Vuga na Kuhudhuriwa na Maji wa Mahakama Kuu Zanzibar, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekhe Khamis Haji Khamis, Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekhe Hassan Ngwali na wajumbe wa tume ya utumishi wa Mahakama. Jaji Mkuu wa Zanzibar akimuapisha Mhe, Fatma Omar Ali kuwa hakimu wa Wilaya. Jaji Mkuu wa Zanzibar akiwa pamoja na Mrajis wa Mahakama Kuu, Manaibu warajis na Mahakimu dhamana na Mahakimu walioapishwa.

current news

Published on /May 6, 2015, 8:08 am/By Hon, George.


KUPANDISHWA DARAJA KWA MAHAKIMU NA MAOFISA SHERIA MAHKAMA KUU ZANZIBAR.

Tume ya Utumishi wa Mahkama chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Jaji Mkusa Sepetu imewapandisha Daraja baadhi ya Mahakimu wa Mahkama ya Wilaya, Mahkama ya Mwanzo na Maofisa Sheria wa Mahkama. Waliopandishwa Daraja kutoka Mahkama ya Wilaya kwenda Mahkama ya Mkoa ni; 1. Mhe. Valentine A. Katema 2. Mhe. Sabra A. Mohamed 3. Mhe. Hussein M. Hussein 4. Mhe. Yahya U. Yahya 5. Mhe. Is-haka A. Khamis, na 6. Mhe. Nayla A. Omeiya Waliopandishwa kutoka Mahkama ya Mwanzo kwenda Mahkama ya Wilaya; 1. Mhe. Asya A. Ali 2. Mhe. Fatma O. Ali 3. Mhe. Luciano M. Nyengo 4. Mhe. Mohamed S. Khamis, na 5. Mhe. Zuwena M. Abdulkadir Maofisa Sheria wa Mahkama walio teuliwa kuwa Mahakimu wa Mahkama ya Mwanzo ni; 1. Mhe. Mohamed A. Haji 2. Mhe. Maulid H. Ali 3. Mhe. Nassim F. Mfaume 4. Mhe. Neema J. Harusi, na 5. Mhe. Rauhiya H. Bakar Uteuzi huo umeanza tarehe 04/05/2015, na Mhe. Jaji Mkuu atawaapisha Mahakimu hao tarehe 06/05/2015 saa nne asubuhi katika ukumbi wa Mahkama Kuu, Vuga. Zanzibar. Tunawapongeza wote katika teuzi hizo, na kuwatakia kila la kheri katika utekelezaji wa majukumu ya Kazi.

current news

Published on /April 8, 2015, 8:22 am/By Mr.Balu.


JAJI MKUU WA ZANZIBAR AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA MAHKAMA ZA PEMBA

Jaji Mkuu wa Zazibar, akiwa na Mrajis wa Mahkama Kuu Mhe George Kazi na Naibu Mrajis wa jimbo Pemba Haji Omar Haji pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Mahkama Kuu Chake chake Pemba. Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Thman Makungu amefanya ziara ya kutembelea Mahkama zilizokuwepo Pemba akizungumza katika ziara hiyo Mhe. Omar Makungu aliwataka Mahakimu wa Mahkama za Ardhi Pemba kuwa makini na baadhi ya watu wanaotumia nyaraka zilizofutwa na serekali mwaka 1964 kudai haki zao za umiliki wa Ardhi Mahkamani. Alisema kumekuwa na watu wanaotumia nyaraka za Mababu zao kufungua madai hasa katika maeneo ya Mashamba wakati tayari Serikali imeshafuta nyaraka hizo, hivyo alisisitiza iwapo Mahakimu hawatakuwa makini Mahkama zitajaa kesi zisizo na msingi na kuchochea Migogoro kwa Wananchi. Aidha Mhe. Jaji Mkuu akizungumzia suala la upandishwaji madaraja kwa Mahakimu unazingatia utendaji Mzuri wa kazi pamoja na kuangaliwa utoaji wa hukumu na si vinginenyo, alisema ili Hakimu aweze kupanda daraja ni lazima aangaliwe uwezo wake wa kufanya kazi na kumaliza kesi kwa wakati. Pia Mhe. Jaji Mkuu alisema ameridhishwa na utendaji kazi wa Mahkama za Pemba hasa katika kupunguza mrundikano wa kesi Mahkamani na kuwaomba Mahakimu na watendaji wengine wa Mahkama kuendelea kufanya kazi Kwa bidii. vile vile Mhe. Jaji Mkuu alipata fursa ya kukagua sehemu inayotarajiwa kufunguliwa Mahkama ya Baraza la Mji Wete na kuzungumza na katibu wa Baraza. Nao kwa upande wao Wafanyakazi wa Mahkama za Pemba walieleza changamoto Mbali mbali zinazowakabili katika utendaji wao wa kazi wa kila siku zikiwemo Uchakavu wa Majengo, ukosefu wa vitendea kazi, na Maslahi madogo wa wafanyakazi, nae Mhe. Jaji Mkuu aliahidi Kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili Wafanyakazi. Katika ziara hiyo Mhe. Jaji Mkuu alifuatana na Mrajis wa Mahkama Kuu Mhe. George Kazi, Naibu Mrajis Mhe. Ali Amer Haji na Maafisa wengine wa Mahkama. Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akikagua eneo linalotarajiwa kuwa ofisi ya Mahkama ya Mwanzo Wete. Jaji Mkuu wa Zanzibar akikagua matengenezo ya Mahkama ya Chake Chake.

current news

Published on /April 1, 2015, 10:18 am/By Mr. Balu.


JAJI MKUU WA ZANZIBAR ATEUA JAJI WA MAHKAMA YA BIASHARA NA NAIBU MRAJIS

Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu amemteua Mhe.Rabia Hussen Mohammed Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar kuwa Jaji wa Mahkama ya biashara, uteuzi huo umekuja baada ya kupitishwa na kusainiwa wa sheria no. 9 ya mwaka 2013 ya kuanzishwa kwa Mahkama ya Biashara. Wakati huo huo Mhe. Jaji Mkuu wa Zanzibar amemteua Mhe.Khamis Ramadhani Abdalla kuwa Naibu Mrajis wa Mahkama ya Biashara uteuzi huo unaanza tarehe 1/04/2015, Mahkama hiyo inatarajiwa kuanza kazi zake katika jengo lililopo pembezoni mwa Mahkama Kuu zamani lilikuwa Maktaba Kuu.

current news

Published on /March 6, 2015, 3:04 pm/By Mr.Balu.


JAJI MKUU AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA MAHKAMA ZA UNGUJA

Jaji mkuu akipata maelezo katika Mahama ya Kadhi waWilaya Mwanakwerekwe. Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othuman Makungu ametembelea Mahakama za Unguja ili kuonana na wafanyakazi na kupata kujua changamoto mbali mbali zinazoikabili Mahakama, akizungumza katika ziara hiyo iliyoanzia Mahakama ya Kadhi wa Wilaya Mwanakwerekwe na kumalizi Mahakama ya Aridh Vuga, Mhe.Jaji Mkuu aliwataka wafanyakazi katika vituo vivyo kufanya kazi kwa bidii, alisema Serekali inazifahamu changamoto wanazokumbana nazo wafanyakazi na inafanya juhudi za makusudi za kuzipatia ufumbuzi changamoto hizi. Pia Mhe, Jaji Mkuu aliwataka mahakimu kuandika hukumu zoa katika hali nzuri kwani miongoni wa sifa za kupanda dara kwa hakimu ni kuandia hukumu zilizonzuri na kuacha tabia ya kuondoa njiani, Nao wafanyakazi wa Mahakama walieleza changomoto mbali mbali zinazowakabili katika utendaji wao wakazi wa kila siku miongoni mwa changomoto walizozieleza ni uchakavu wa Majengo, kuchelewa kupatikana vifaa vya kutendea kazi, mishahara midogo,ukosefu wa usafiri. Katika ziara hiyo Jaji Mkuu alifuatana na Mrajis wa Mahakama Kuu,naibu Mrajis na maofisa mbali mbali wa mahakama. Jaji Mkuu wa Zanzibar akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mahakama ya Mkoa Mkoa Mwara. jaji Mkuu akipata maelezo wakati alipotembelea Mahakama ya Wilaya Mkokotoni. Jaji Mkuu akikagua Jengo la Mahakama ya Wilaya Makunduchi.

current news

Published on /February 12, 2015, 2:36 am/By Mr.Balu.


DK. SHEIN MGENI RASMI SIKU YA SHERIA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapiduzi Dk Ali Mohammed Shein akitoa hutuba yake katika siku ya sheria Zanzibar. Raia wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein, alisema kuwepo kwa uwazi katika kusikiliza Mashauri ya kesi katika mahakama mbali mbali nchini kutarejesha imani kwa wananchi juu ya Mahakama kwani wananchi walikuwa tayari wamepoteza imani na Mahakama. Pia alisema wananchi bado hawako tayari kwenda mahakamani kutoa ushahidi hali ambayo inapelekea kuchelewa kutolewa kwa uamuzi wa kesi mbali mbali hasa ya unyanyasaji wa kijinsia. Aidha alisema Majaji , Mahakimu na Wanasheria wana jukumu la kuhakikisha kampeni ya unyanyasaji wa kijinsia kwani bado kuna changamoto kubwa katika kutimiza matarajio ya wananchi hasa katika uendeshaji wa kesi za udhalilishaji ambapo zipo lawama na malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya usimamizi na uendeshaji wake. Mbali na hayo Dk shein alimpongeza jaji mkuu wa Zanzibar pamoja na uongozi wake wa mahakama kwa uamuzi wao wa kujiunga na jumuiya ya majaji na mahakimu ya Afrika mashariki ikiwa ni mwanachama wa kushirikishwa. Alitoa wito wa kuongezwa kasi ya kuanzishwa mahakama ya biashara ili kuimarisha sekta ya biashara nchini. Pia katika sherehe hizo Dk shein alizidua kitabu cha "Zanzibar year book of law volume three", Nae kwa upande wake Jaji mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othuman Makungu alisema kauli mbiu ya mwaka huu MAHAKAMA HURU MSINGI WA UTAWALA BORA ni kutokana na kuzingatia kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu na upigaji wa kura ya maoni juu ya katiba inayopendekezwa, hivyo mahakama imejipanga vyema kushuhulikia mashauri yoyote yatakayofikishwa mbele ya mahakama kuhusu uchaguzi, na majaji na mahakimu watatenda haki kwa mujibu wa sheria za nchi na hawatajiingiza katika ushabiki wa kisiasa. Pia Mhe.Jaji Mkuu alimpongeza Dk shein kwa jitihada mbali mbali anazozichukua katika kutatua changamoto zinazoikabili mahakama kwa mfano alisema Dk shein ni rais wa kwanza toka Mapinduzi ya mwaka 1964 kuchagua Majiji watano na jaji mkuu, kuchagua kadhi mkuu na naibu kadhi mkuu na makadhi wote isipokuwa makadhi watatu tu katika kipindi chake cha uongozi. Pia Mhe, jaji mkuu alisema mahakama inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ufinyu wa bajeti idadi ndogo ya majiji ambapo alisema iwapo katiba mpya ikipita kutahitajika majaji zaidi kutoka Zanzibar kuingia katika mahakama ya juu. Kwa upande wake waziri wa katiba na sheria Mhe. Abubakar Khamis Bakari alisema maana halisi ya uhuru wa mahakama kwa msingi wa utawala bora ni kuwa na nguvu, uwezo na uhuru katika kuwatumikia watu, alisema katika karne hii ya utandawazi na hali uchumi ni lazima Mahakama zibadilike na zijikite zaidi katika kuwatumikia watu kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa. Nae mwanasheria wa mkuu wa serekali Mhe. Said Hassan Said alisema utoaji wa haki unapokuwa hauna uadilifu ,haufuati msingi wa usawa na utawala wa sheria unaweza kusababisha hata ufinyu wa amani na dhana nzima utawala bora hupotea. Nae Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Mhe. Ibrahimu Mzee alisema uhuru wa Mahakama sio zawadi bali ni msingi wa kikatiba na ni msingi wa utawala bora unaoandamana na jukumu kubwa la mahakama la utoaji wa haki Kwa upande wake Rais wa chama cha mawakili Zanzibar Awadh Ali Said alisema wakati sasa umefika kuwa na mfuko wa mahakama ambao unatumika kwa shuhuli za uendeshaji wa mahakama, aidha alisema ni jukumu la serekali kutenga fedha za kutosha katika kila mwaka wa bajeti na kuingia katika mfuko huo mahakama. Pia alisema wakati sasa umefika wa mahakama kuwa na mtendaji mkuu wa mahakama, alisema nchi ambazo tayari zimetumia mfumo huu wa kuwa na mtendaji mkuu wa mahakama zimepiga hatua katika sekta ya mahakama. Sherehe hizo za kuadhimisha siku ya sheria Zanzibar kwa mara ya nne zimefanyika katika viwanjwa vya Victoria Garden na kuhudhuriwa na makamo wa pili wa rais wa Zanzibar Balozi seif ali Iddi, Jaji mkuu wa Tanzania Mhe. Mohammed Chande Othuman, Jaji Kiongozi Mhe. Shaaban Ali Lila, naibu sipika wa baraza la wawakilishi Mhe. Ali Abdalla, kadhi mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Naibu Kadh Mkuu wa Zanzibar sheikh Othuman Hassan Ngwali na viongozi mbali mbali wa serekali. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa bara la mapiduzi Dk Ali Mohammed Shein akionyesha kitabu alichokizindua katika sherehe za siku ya sheria. Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Omari Othuman Makungu akisoma hutuba yake katika siku ya sheria Zanzibar. Mhe.jaji mkuu wa Tanzania na naibu sipika wa baraza la wawakilishi wakiwa katika siku ya sheria Zanzibar . Kadhi mkuu wa Zanzibar sheikh Khamis Haji na naibu kadhi wakiwa na makadhi wengine katika siku ya sheria Zanzibar.

current news

Published on /January 29, 2015, 2:31 pm/By Mr. Balu.


TANGAZO LA KONGAMANO

MAHKAMA KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA SHERIA ZANZIBAR IMEPANGA KUFANYA KONGOMANO SIKU YA ALKHAMIS TAREHE 5 FEBRUARY 2015 KUANZIA SAA 2:30 ASUBUHI KATIKA UKUMBI WA STUDIO ZA MUZIKI NA FILAMU RAHALEO. KONGAMANO HILO LITAKUWA NA KAULI MBIU INAYOSEMA "MAHKAMA HURU MSINGI WA UTAWALA BORA" HIVYO WANANCHI WOTE MUNAALIKWA NA KUOMBWA KUHUDHURIA KATIKA KONGAMANO HILO.

current news

Published on /January 22, 2015, 2:02 pm/By Mr.Balu.


JAJI MKUU AWAAPISHA MAULAMAA WA MAHKAMA KUU YA ZANZIBAR.

Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe, Omar Othuman Makungu aliwataka maulama kutambua kuwa wao ni msada mkubwa kwa Majiji ili kuweza kutenda haki na uadilifu katika maamuzi ya kesi hasa za mirathi, na talaka, . Pia Mhe. Jaji Mkuu wa Zanzibar aliwapongeza maulamaa hao kwa kukubali kwao kuwa maulamaa wa mahkama kuu, kwani mwazo watu walikataa kuwa maulamaa. Nae Shekhe Hilali akitoa salamu kwa niaba ya maulamaa wenzake alisema watafanya kazi yao ya ulamaa kwa kuzingatia misingi ya sheria zilizopo, na pia aliishikuru tume ya utumishi wa Mahkama kwa kuwaamini na kuwateuwa kuwa maulamaa wa Mahkama kuu ya Zanzibar. Hafla ya kuwaapisha maulamaa hayo ilifanya katika ukumbi wa Mahkama Kuu Vunga na kuhudhuriwa na Majaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar, Kadhi Mkuu wa Zanzibar na Wajumbe wa tume ya Utumishi wa Mahkama , jumla ya maulamaa kumi na nne kutoka Unguja na Pemba waliapishwa na Mhe. Jaji Mkuu wa Zanzibar.

current news

Published on /December 9, 2014, 12:10 pm/By Mr.Balu.


DK SHENI AMUAPISHA JAJI MKUSA KUWA KAIMU JAJI MKUU WA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Ali Mohd Sheni amemuapisha Jaji Mkusa I. Sepetu kuwa kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar, hafla hiyo ilifanyika katika Ikulu ya Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serekali akiwemo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Ikulu na Utawala bora Mhe.Mwinyi Haji Mkame,Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Abdallah Mwinyi Khamis, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji na viongozi wengine wa Serekali ya Zanzibar.

current news

Published on /December 1, 2014, 8:45 am/By Mr.Kipevu/Hinji.


MAHAKAMA YA RUFAA ZANZIBAR

MAHAKAMA ya Rufaa Tanzania Kanda ya Zanzibar imeanza vikao vyake ambapo Mashauri 22 yatasikilizwa na kutolewa maamuzi yakiwemo rufaa za Jinaii na Madai yatakayosikilizwa na Majaji watatu. Akizungumzia kikao hicho cha Mahakama ya Rufaa Naibu Mrajis Mahakama ya Rufaa Mhe, Francis Jacob Kabwe amesema mashauri hayo tisa ni rufaa za madai matano jinai na mashauri mengine ni maombi ya madai na moja la jinai. Mhe Kabwe amesema vikao hivyo vinaongozwa na Majiji watatu chini ya Mwenyekiti wake Jaji Nathalia Kimaro Jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania na kumalizika tarehe 12 mwezi huu. Kabla ya kuanza kwa vikao hivyo Jaji Nathalia Kimaro alikagua paredi rasmi la jeshi la Polisi kuashiria kuanza kwa Mahakama ya Rufaa Kanda ya Zanzibar ambapo kikao hicho hufanyika mara moja kwa Mwaka. Baadhi ya rufaa zitakazosikilizwa ni Madai ya Machano Khamis Ali na wezake 17 dhidi ya Kamishna wa Polisi Zanzibar na wezake wawili na rufaa nyengine.

current news

Published on /November 20, 2014, 2:41 pm/By Mr.Balu.


JAJI MKUU AWAKABIDHI MAWAKILI WAPYA VYETI

Jaji Mkuu wa Zanzibari akisoma hotuba yake katika sherehe ya kuwakabidhi mawakili wapya vyeti. Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Othman Omar Makungu amewataka Mawakili wapya kufanya kazi zao za uwakili kwa kufuata katiba,sheria na maadili ya kazi hiyo na kuweka mbele maslahi ya Umma mbele kuliko maslahi binafsi."Najua kutokana na upya wenu baadhi yenu mtakuwa na woga wa kuja na kesi Mahakamani lakini hili naomba lisiwarudishe nyuma, kwani naamini uwezo wa kufanya vizuri mnao". Pia Jaji Mkuu alisema Inasikitisha kuona kuwa baadhi ya Majaji, Mawakili, na Mahakimu hawafuati maadili ya kazi na kujiingiza katika mambo ya rushwa, utovu wa nidhamu ubinafsi na mengineyo. Aidha alisema Mawakili kuahirisha kesi bila ya sababu za msingi hili si sawa mbele ya jamii na mbele ya Mungu. Vile vile Jaji Mkuu alisema Inasikitisha kusikia baadhi ya Majaji au Mahakimu kupendelea baadhi ya Mawakili na kuwachukia baadhi ya wengine, alisema Haya yote ni mambo mabaya na yanapaswa kuyapiga vita kwa nguvu zote ili haki iweze kupatikana. Pia alisema Ili kufanya haki hawana budi kujiepusha na mambo yarushwa, kujuana, udugu, urafiki, ukabila, ujimbo n.k. Aidha Mhe Jaji Mkuu alisema, Hivi sasa kuna malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na wenye kesi kuwa Mahkama inachelewesha sana kesi, alisema Kwa upande mmoja malalamiko haya yana ukweli na ucheleweshaji huo unachangiwa na mambo mbali mbali akiyataja baadhi ya mambo hayo kuwa ni Pingamizi za awali (Preliminary objections), Kutajwa kwa kesi bila ya sababu (Mention) Uakhirishaji wa kesi (Adjournment) na Kutokamilika kwa upelelezi/kutopatikana kwa mashahidi. Nae Mwakilishi wa Mwanasheria mkuu wa serikali bwana Saleh Mbaraka aliwapongeza mawakili hao wapya kwa jitihada waliochukua toka wanasoma hadi kuwa mawakili, alisema kuwa kazi ya sheria si kazi ya lelemama kwa sababu kazi ya sheria lazima uwe na uwezo wa kufikiri kwa haraka na uwezo wa kuamua kwa haraka, vile vile alisema kazi kubwa ya wakili mahakamani si kushindana na Jaji au Hakimu bali ni kujenga hoja za kisheria ambazo zitakubalika. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Bwana Ibrahimu Mzee alisema , si vyema kwa wakili wala kwa mahakama wala kwa hadhi na heshima ya utawala wa sheria na wala kwa utowaji wa haki kwa wakili kumhoji shahidi kwa maswali au ya kukasirisha, alisema kumhoji shahidi kwa maswali ya matusi na yakukasirisha ni jambo ambalo linakatazwa kwa mujibu wa kifungu cha 152 cha sheria ya ushahidi sura ya 5 sheria za Zanzibar. Vile vile Mkurugenzi wa mashtaka aliwakumbusha mawakili wapya makatazo yaliyomo kwenye sheria ya mawakili ya Zanzibar yaani legal practitioners decree sura ya 28 ya sheria ya Zanzibar, akiyataja makatazo hayo kuwa ni wakili kuwa na maslahi yoyote kwenye kesi ya mteja wake na wakili asiwe anatoza ada (fees) kulingana na matokeo ya kesi. Nae katibu wa chama cha wanasheria Zanzibar bwana Omar Said Shaaban alisema kazi ya uwakili ni kazi ngumu na inayohitaji umakini, alisema umakini unahitajika kwa kuwa wakili ana wajibu wa namna mbili kwanza ni kwa mteja wake anapaswa kumlinda na kumtetea kwa ujuzi na maarifa ili kuhakikisha kuwa haki yake iliyopotea au iliyo katika hatari ya kupotea inalindwa na wajibu wa pili wa wakili ni kama Afisa Mahakama kumsaidia Jaji au Hakimu kutenda haki kulingana na sheria. Jaji Mkuu wa Zanzibar akiwa katika picha ya pamoja na mawakili wapya aliowakabidhi vyeti. Majaji wa Mahakama kuu Zanzibar wakisikiliza Hotuba ya Jaji Mkuu wa Zanzibar . Jaji Mkuu wa Zanzibar akimkabidh cheti chake wakili mpya.

current news

Published on /November 12, 2014, 4:00 pm/By Mr. Balu.


JAJI MKUSA AFUNGUA MAFUNZO YA SIKU TANO YA MAJAJI NA MAHAKIMU WANAOSHUHULIKIA KESI ZA WATOTO.

Mhe.Mkusa I. Sepetu akifungua mafunzo ya Majaji na mahakimu wanaoshuhulikia kesi za watoto. Jaji wa Mahakama kuu Zanzibar Mhe. Mkusa I. Sepetu Amesema kuanzishwa kwa sheria mpya ya watoto kutatua wigo mpana wa namna bora ya kushuhulikia masuala yote yanayohusu mtoto, aidha alisema sheria ya mtoto ni kwa ajili ya mtoto tu na ina utaratibu wake wa kumshuhulikia mtoto anapofikishwa mahakamani ukilinganisha na sheria nyengine. Pia Mhe. Mkusa alisema Serikali ya Mapindizi ya Zanzibar imeanzisha sheria ya Mtoto No 6.ya 2011 ambayo inatamka wazi kwamba mtoto ni mtu ambaye umri wake hauzidi miaka kumi na nane pia kuna haki mbali mbali za watoto zimeanzishwa ndani yake, pia Mahakama ya watoto imeanzishwa kwa lengo la kuwashuhulikia watoto pomoja na utaratibu wake umeelezwa bayana katika sheria hiyo. Vile vile Mhe. Mkusa aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kuwa makini na kuyazingatia mafunzo yanayotolewa kwani alisema kuazishwa kwa sheria hiyo mafanikio mbali mbali yameanza kufikiwa aliyataja mafanikio hayo kuwa ni kufunguliwa kwa Mahakama ya wototo tarehe 5/2/2013 na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othuman Makungu, na matayarisho ya kufungua mahakama kama hiyo kwa upande wa Pemba yako mbioni na muda wowote kuanzia sasa Mahakama hiyo itafunguliwa kwa upande wa Pemba. Mafunzo hayo yamefanyika katika hotel ya Visitors Inn Jambiani na kufadhiliwa na unicef kwa kushirikiana na mahakama Zanzibar na kuhudhuriwa na Majaji na Mahakimu wa Unguja na Pemba Majaji wa Mahakama kuu Zanzibar Mhe. Mkusa na Mhe Rabia wakiwa pamoja na mtoa mada wa mafunzo ya majaji na mahakimu Jambiani. Naibu Mrajis wa Mahakama kuu Mhe.Khamis Ramadhani wakati wa wafunzo wa Majaji na Mahakimu huko Jambiani. Mwenyekiti wa Mahakama ya watoto Mhe. Sabra Ali akiwa pamoja na Mhe. Valentina na Mhe. Khamis wakisikiliza ufunguzi wa mafunzo.

current news

Published on /October 21, 2014, 9:30 am/By Mr Balu.


JAJI MKUU AWAAPISHA MAKADHI WA WILAYA WAPYA

Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othuman Makungu amewaapisha makadhi wa Wilaya wapya walioapishwa ni Shekh Abubakar Ali Mohd, Shekh Ali Haruna Ramadhan,Shekh Mohd Ramadhan Khamis na Shekh Omar Juma Othuman.Makadh hawa wameapishwa kwa kujaza nafasi zilizowachwa wazi na makadh waliostaafu kwa mujibu wa sheria. Akizungumza baada ya kuwaapisha Mhe.Omar Othuman Makungu aliwataka kufanya kazi kwa mujibu wa sheria kwani alisema kazi ya utowaji wa haki ni kazi ambayo inatekelezeka ikiwa watatenda kazi zao kwa mujibu sheria na kuzingatia maadili ya kazi, nao makadh wapya walisema watafanya kazi zao za ukadhi wa wilaya kwa kuzingatia haki na sheria inayowaongoza. Hafla hiyo ilifanyika Ofisini kwa Jaji Mkuu na kuhudhuriwa na Naibu kadhi Mkuu Shekh Hassani Othumani Ngwali,kadhi wa Rufaa Pemba Shekh Daudi, naibu warajis wa Mahakama Kuu na baadhi ya Mahakimu. Jaji Mkuu wa Zanzibar Akimuapisha Shekh Abubakar Ali Mohd kuwa kadhi wa wilaya. Jaji Mkuu wa Zanzibar akimuapisha Shekh Omar Juma Othuman kuwa kazi wa wilaya. Jaji Mkuu wa Zanzibar akimuapisha Shekh Ali Haruna Ramadhan kuwa kadhi wa wilaya. Jaji Mkuu wa Zanzibar akiwa na majaji wa Mahakama Kuu na Makadh wapya wa Wilaya aliyowaapisha.

current news

Published on /October 15, 2014, 12:00 am/By Mr Balu.


KONGAMANO LA MAJAJI LAFANYIKA NAIROBI KENYA

Kongamano la Mwaka la Majaji, Mahakimu na Makadhi wa nchi za Afrika Mashariki lafanyika mjini Nairobi , Kenya. Kongamano hilo linaloambatana na Mkutano Mkuu wa Jumuia ya Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki ( East African Magistrates and Judges Association "EAMJA") limefunguliwa Rasmi jana na Raisi wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta. Kauli mbiu ya Mkutano huo ni " Administration of Justice in the Region: Reflections and perspective " . Jumla ya mada Sita zitajadiliwa katika kongamano hilo nazo ni 1. Constitutionality sanctioned principle of separation of powers 2. Justice Sector collaboration in the Administration of justice: Judges' and Magistrates' collaboration/ cooperation with: other arms of government; and stakeholders 3. Protection of the rights of children ,women and the elderly : from frameworks to coordination 4.The relationship between the EACJ and the National Courts 5. Transnational Organised Crimes : what are the threats in the region, what are the relevant protocols, laws and mechanisms, and how can the EAC extend its internal cooperation to fight these crimes? Na 6. Court Management : Reflections on coordinated Approaches to Leadership, case management and IT support. Kongamano hilo limeanzia tarehe 13 Octoba 2014 na kumalizika tarehe 18 Octoba 2014 limeshirikisha Watendaji zaidi ya 300 Kutoka nchi za Tanzania (Bara na Zanzibar) Kenya ,Uganda, Rwanda, Lesotho, South Sudan na Mahakama ya Afrika Mashariki wa kiongozi na Majaji wakuu wa nchi hizo, pamoja na taasisi mbali mbali kama ICJ Kenya, ICC na UNDP .


Ujumbe kutoka Zanzibar uliongozwa na Jaji Mkuu Mhe. Omar Othman Makungu.

current news

Published on /September 28, 2014, 12:00 am/By Balu.


Mkutano wa Majaji wa Afrika Mashariki wafanyika Zanzibar

Mkutano uliohusisha Baadhi ya Majaji na Mahakimu wa Mahakama za Afrika Mashariki unaohusiana na Mikakati ya kupiga vita masuala ya kigaidi na uhalifu wa kimataifa umefanyika Zanzibar kwa siku 5 kuanzia tarehe 22 Septemba 2014 na kumalizika tarehe 26 Septemba 2014. Mkutano huo ulifunguliwa na Mhe Jaji Mkuu wa Zanzibar katika hotel ya La Gema, Nungwi Zanzibar. Katika Mkutano huo Mahkama Kuu ya Zanzibar iliwakilishwa na Mhe. Jaji Mkuu, Mhe Omar O Makungu, Mhe.Jaji Mshibe Ali Bakari, Mhe. Jaji Fatma H Mahmoud, Naibu Mrajis wa Mahkama Kuu Mhe Yessaya Kayange na Mhe. Khamis Ramadhani, pamoja na Hakimu wa Mkoa Mhe Mohamed Ali Mohamed ? Mhe Jaji Mkuu wa Zanzibar katika picha ya pamoja na washiriki wa Mkutano huo. Jaji Mkuu wa Zanzibar akiwa na Jaji Mkuu wa Sudani ya Kusini Mhe. Chaan Madut wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo Washiriki kutoka Zanzibar wakifuatilia hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na Mhe Jaji Mkuu wa Zanzibar.

current news

Published on /September 10, 2014, 12:00 am/By Balu.


MRAJIS WA MAHKAMA KUU AFUNGUA MAFUNZO YA SIKU MOJA YA MAKARANI WA MAHKAMA .

Mrajis wa Mahkama kuu Mhe . George Kazi amewataka makarani kujitambua na kuelewa majukumu yao vizuri kwani wao ni watumishi muhimu katika Mahakama kama Taasisi inayosimamia sheria na usimamizi wa haki, alisema bila ya Makarani kazi za Mahkama zinaweza kulala. Pia Alisema kuwa watendaji wengi serikalini hawaijui nafasi ya karani hivyo mafunzo haya yatatoa mwanga kwa makarani na ujumbe kwa watu wananchi wengine. Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo cha huduma za Sheria Zanzibar Bibi Harusi M. Mpatani aliwataka Makarani pindi atapokwenda mtu Mahkamani kutaka msada wa kisheria wamuelekeze kituo cha Huduma za sheria kwani wanaamini wananchi wengi wa Zanzibar hawana uwezo kisheria na hata uwezo wa kifedha wa kulipa Mawakili. Mafunzo hayo yalikuwa na lengo la kuwajengea uwezo zaidi juu ya haki za binaadamu na utawala bora na pia kuwakumbusha makarani hao wajibu wao wa kazi na maadili ya kazi zao. Mada nne ziliwashwa katika mafunzo ambazo ni Kujitambua kwa Karani, Umuhimu wake kazini, Uadilifu na Maadili ya Karani (ethics), : Utayarishaji na Utowaji wa Hati Mbali mbali ya Mahakama- Decrees, Drawn Orders, na Summon warrant, Umuhimu wa Karani katika Utunzani wa Majalada na Kumbu kumbu mbali mbali na Nafasi ya Makarani kwa Mujibu wa Sheria- Stahiki zao na Maslahi mengine Mafunzo hayo yaliyofanyika jumamosi tarehe 06 Septemba 2014 yaliandaliwa na kituo cha huduma za sheria Zanzibar yalifanyika katika ukumbi wa Kituo hapo Migombani na kuhudhuriwa na Makarani kutoka Mahkama tofauti za Unguja.

current news

Published on /September 4, 2014, 12:00 am/By Balu na Maulid Kipevu.


JAJI MKUU AKUTANA NA WAKUU TAASISI ZA SHERIA

Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe, Omar Othman Makungu amekutana na Watendaji wakuu wa taasisi zinazoshirikiana katika kuendesha shughuli zao pamoja katika kuwahudumia wananchi mambo ya kisheria ikiwemo kesi za jinai. Jaji Mkuu amekutana na Kamishna wa Polisi Zanzibar , Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Mkurugenzi wa Mashtaka pamoja na Kamishna Vyuo vya Mafunzo Zanzibari huko ofisini kwake Vuga kujadili masuala mbali mbali kuhusiana na kazi zao. ?Mhe jaji Makungu amesema kuna umuhimu kwa viongozi hao kukutana, kujadili na kutizama mambo mbali mbali katika kutekeleza vyema wajibu wao hasa wakati huu ambao zipo changamoto nyingi zinazohitaji kukaa na kuzifanyiakazi kwa pamoja. Akizungumza baada ya kikao hicho Mrajisi wa Mahakama Mhe George Kazi amesema hii ni mara ya kwanza kukutana pamoja Viongozi wa taasisi hizo na lengo kuu lilikuwa ni kujuwana na kuangalia mikakati ya kuimarisha kwenye mapungufu katika usimamizi wa sheria na utekelezaji wake kwa pamoja . Wazo la kukutana Viongozi hao liliibuka wakati Kamishna wa Polisi Kamanda Hamdan alipokwenda kujitambulisha kwa Mhe Jaji Mkuu mara baada ya uteuzi wake. Mhe George amesema katika kikao hicho kimesisitiza mwendelezo wa Kamati ya kusukuma kesi kwa lengo la usimamizi mzuri wa kesi za jinai ikiwemo kuangalia namna ya kutafuta mikakati ya kupunguza mrundikano wa kesi na kupunguza malalamiko ya wananchi ambayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara. Kikao hicho kimepangwa kufanyika kila baada ya miezi mitatu Jaji Mkuu akiwa na Wakuu wa Taasisi za Sheria katika kikao hicho. Kamishna wa Chuo cha Mafunzo akifuatilia kwa makini kikao hicho.

JAJI  MKUU AKUTANA NA WAKUU TAASISI ZA SHERIA

current news

Published on /September 4, 2014, 12:00 am/By Maulid Kipevu.


Mahakimu Wafanya Ziara Chuo Cha Mafunzo Kilimani.

Wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo (Wafungwa) na Mahabusu wameiomba Serikali kutafuta adhabu mbadala za kutumikia jamii kwa wanafunzi wanaopatikana na hatia kwa makosa madogo madogo ili kupunguza msongomano wa wanafunzi pamoja na Mahabusu gerezani . Wakizungumza katika ziara ya Mahakimu wa Mahakama mwanafunzi Muhammed Hamza kwa niaba ya wezake amesema katika kuzingatia haki za binaadam yako makosa mengi ambayo Serikali ingalikaa na kuyatizama upya na kuyatafutia adhabu zitakazolingana na makosa hayo. Hamza aliyataja baadhi ya makosa hayo kuwa ni wizi wa mazao, kuku nk ambapo alitoa mfano wa nazi mbili mtu anawekwa rumande miezi sita wakati kifungo chake inawezekana ikawa miezi miwili na mengine kama hayo. Mwanafunzi huyo alitaja kutokuwepo kwa usawa wa sheria na kudai kwamba mara nyingi kunakuwa na viashiria vya rushwa katika upatikanaji wa haki na kwamba chuo cha mafunzo ni sehemu ya asokuwa nacho na mwenye nacho hastahiki, alisema pia sheria hutumiwa kutizama upande mmoja na upande mwengine kutofanyakazi wakati sheria haina mkubwa. Alisema kuhusu upatikanaji wa mwenendo wa kesi mara zinapomalizika kwa kesi bado limekuwa tatizo sugu na kuchukuwa muda mrefu na hata waombaji kukata tamaa ya kukosa haki zao za msingi kupitia Mhimili huo wa Mahakama. Kuhusu utaratibu wa upatikanaji wa dhamana ya rufaa kwa wanafunzi (wafungwa) wanaohukumiwa adhabu gerezani kuwa bado ni shida kupatikana, wakati sheria ipo na mtuhumiwa anaweza kubaki nje hadi rufaa yake itakapomalizika. Akizungumzia dhamana za kawaida kwa kesi zilizopo Mahakamani washitakiwa waliopo Rumande wamedai kuwa upo ubaguzi kwa wazanzibari na wazanzibara na vigezo wanavyowekewa ni vile ambavyo vinalenga kuwapa adhabu na sio haki za kisheria zilivyo. Muhammed Hamza akitoa baadhi ya mifano kuwa kutolewa dhamana kwa Mansoor Yussuf Himid kwa kosa aliloshitakiwa nalo na wengine kubaki mahabusu kwa makosa ya aina moja ni ubaguzi, kutakiwa wadhamini watumishi wa Serikali wakati mwengine kunawanyima haki watuhumiwa walio wengi ambao hawana jamaa ambao ni watumishi wa serikali. Madai mengine yaliyotolewa ni kuchelewa kwa kuanza kwa kesi Mahakamani na Mahakimu kutofanyakazi siku za Ijumaa wakati Mahabusu wanateseka gerezani na utaratibu wa kuwaita mashahidi hauko mzuri na kuchangia kesi kuwepo kipindi kirefu. Gangira Chaleas ambae ni Mahabusu alitilia mkazo suala la haki ya dhamana kwa watuhumiwa na kunukuu Nakala ya gazeti la Mwananchi lililoandikwa kesi ya aliyekuwa Waziri wa SMZ Mansoor Yussuf Himid kupewa dhamana kwa kosa aliloshitakiwa nalo na wengine kubaki mahabusu kesi nyengine ni kesi za dawa za kulevya ambazo watuhumiwa wanamaliza Miaka bila kesi zao kumalizika kwa wakati na watuhumiwa kukaa ndani zaidi ya mwaka mmoja. Gangira alishauri kwa Serikali kuandaliwa utaratibu utakaowezesha kesi zikasikilizwa kwa wakati ili haki zipatikane kwa wenye haki tena kwa wakati, na dhamana zikitolewa kwa kufuata utaratibu na sheria mrundikano gerezani unaweza kwisha na Serikali haitakuwa na mzigo wa kuhudumia watu ambao wanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Taifa kwa kufanyakazi na kulipa kodi. Wanafunzi hao na rumande wakizungumzia vitendo vya unyanyasaji dhidi ya Watuhumiwa wanapokamatwa na kufikishwa vituo vya Polisi wamedai kufanyiwa vitendo ambavyo haviendani na haki za binaadamu pamoja na kupoteza mali zao ambazo wanaziweka Polisi. Gangira alisema kuwa vitendo vingine wanavyofanyiwa Polisi ni mateso bila ya kupatiwa matibabu wanapopata majeraha na vitendo vya udhalilishaji kinyume na haki za binaadamu. Aidha wamemuamba mrajisi wa Mahakama kuandaa utaratibu wa Kamishna wa Polisi Zanzibar kutembelea gerezani na watendaji wake kusikia kilio chao ili kuweza kupatiwa ufumbuzi utakaosaidia kupatikana kwa haki. Mahabusu hao kwa pamoja wametaja matarajio yao makubwa ya kufanyiwa kazi malalamiko yao ili kuona kilio chao cha muda mrefu kinaisha na sheria kufuata mkondo wake na wamesema hawana lengo la kujenga chuki kati ya watendaji hao na Mahakimu lengo lao ni kujenga misingi imara ya kuendeleza kazi zao. Akijibu baadhi ya malalamiko ya Wanafunzi (Wafungwa) na Mahabusu Mrajis wa Mahakama Kuu Ndugu George Kazi alisema ziara yao wamejifunza mambo mengi ikiwemo kuona hali halisi ya Wafungwa na Mahabusu wanavyoishi gerezani. Mrajis alisema amepokea malalamiko yao na atayafanyia kazi. Akizungumza kuhusu kuhusu dhamana ya Mansoor alisema uamuzi wa Mahkama Kuu umefunguwa mlango kwa watuhumiwa wengine kutumia kifungu cha 150(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Jinai ya mwaka 2004 kuomba dhamana ili nao wapate haki hiyo. Mrajis alisema tokea sheria hiyo ianze miaka kumi iliyopita kifungu hicho cha 150(4) hakijawahi kutumiwa hapa Zanzibar na Mansoor ndiye wa mwanzo kuiomba Mahkama kutumia kifungu hicho hivyo wengine nao watumie fursa hiyo. Kuhusu malalamiko ya shutuma kwa Mahakimu na kujihusisha na vitendo vya rushwa na kutotenda haki ameahidi kulifanyia kazi kuyaondosha malalamiko hayo na suala la dhamana litaangaliwa. Kuhusu kupatikana kwa mweneno wa kesi na hukumu amesema tatizo ni miundombinu lakini tayari tatizo hilo linafanyiwa kazi. Ndugu George Kazi amewaomba wanafunzi na rumande kuisaidia Mahkama kwa kueleza kasoro zote wanazoziona kwa watendaji wake ili Uongozi uweze kuziondoa changamoto ambazo zipo na kuonekana kuwa ni kero kwa jamii ambapo Wanafunzi(Wafungwa) na Mahabusu ndio wadau wakuu . Amewataka wote wenye kesi zilizosikilizwa lakini hukumu haijatolewa muda mrefu kuwasilisha malalamiko hayo kwake ili aweze kuyafanyia kazi. Awali Kamishna wa Vyuo vya Mafuzo Khalifa Haji Chum alisema ujio wa Mahakimu kutasaidia kuleta ufanisi na mashirikiano katika taasisi hizo muhimu ambazo zimebeba jukumu kubwa la kusimamia sheria za nchi. Kamishna Khalifa amesema ziara za watendaji wanaohusika na moja ya majukumu yao kunasaidia kuona wapi kwenye mapungufu na kuyafanyiakazi ili kudumisha amani katika nchi ambayo ndio dira ya maendeleo. Mapema Msaidizi Kamishna wa Vyuo vya Mafunzo Haji Vuai Usi alisema wapo wanafunzi 169 na Mahabusu 234 wakiwepo mfungwa mmoja mwanamke na watano mahabusu, watoto watano. Nao Mahakimu waliotembelea gereza kuu la Kiinua Miguu wamesema wamejifunza mambo mengi katika ziara hiyo na kuiomba serikali kutoa ushirikiano wa kutosha kwa taasisi hizi ili kupunguza au kuondosha kabisa matatizo yaliyopo ikiwemo miundombinu.

current news

Published on /July 23, 2014, 12:00 am/By Balu.


ZANZIBAR JUDICIAL OFFICERS ASSOCIATION (ZAJOA) YAANDAA MAFUNZO YA SIKU MOJA KWA MAJAJI,MAHAKIMU NA MAKADHI

Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe, Omar Othuman Makungu amewataka Majaji na Mahakimu kuwa na utaalamu mzuri ili waweze kutoa hukumu yenye kuzingatia haki kwa jamii. Alisema, hukumu ni kitu muhimu sana cha kuzingatiwa kwa sababu ndio hatua ya mwisho ya kuhakikisha kila mmoja anapata haki yake inayomstahiki kwa misingi ya sheria iliyopo. Aidha, alisema utoaji mbaya wa hukumu kwa kufuata matakwa binafsi unapelekea jamii kutokuwa na imani na Mahkama. Mhe Omar Othman Makungu aliyasema hayo katika ufungaji wa Mafunzo ya siku moja yaliyofanyika katika Mahkama Kuu Vuga yaliyoandaliwa na ZAJOA. Naye Rais wa ZAJOA Mhe. Jaji Abraham Mwampashi alisema mafunzo hayo ni mwanzo wa mafunzo mengine ya kujenga uelewa zaidi kwa Majaji, Makadhi na Mahakimu. Mada mbili siliwasilishwa katika mafunzo hayo yaliyofanyika tarehe 19 Julai 2014 katika ukumbi wa Mahkama Kuu Vuga, ambazo ni RECORDING OF EVIDENCE iliyowakilishwa na Mhe. Jaji Abraham Mwampashi na CONTENTS OF JUDGMENT iliyowasilishwa na Mhe George Kazi, Mrajis wa Mahkama Kuu Zanzibar. Jaji wa Makhama kuu Zanzibar Mhe, Abraham Mwampashi akitoa mada ya Recording of Evidence katika Mafunzo Majiji, Mahakimu na Makadhi yaliyofanyika ukumbi wa Mahkama Kuu Vuga. Mrajis wa Mahkama Kuu Mhe, George Kazi akiwasilisha mada ya Contents of Judgment katika mafunzo ya Majaji, Mahakimu na Makadhi. Majaji Mahakimu na Makadhi wakiwa katika mafunzo ya siku moja katika ukumbi wa Mahkama Kuu Vuga.

current news

Published on /July 15, 2014, 12:00 am/By Mrajis.


Jaji Mkuu Afutarisha Watendaji wa Mahkama Unguja

Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu afutarisha watendaji wa Mahkama Kuu na Mahkama nyinginezo za Unguja. Katika hafla ya futari hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Salama katika Hotel ya Bwawani siku ya tarehe 13 Julai 2014 pia ilihudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Abubakary Khamis Bakari pamoja na watendaji wa taasisi mbalimbali zinazoshughulika na usimamizi wa haki Zanzibar. Mhe Jaji Mkuu Mhe Omar Othman Makungu akiwaongoza wageni wake katika hafla hiyo. Jaji Mkuu Mhe Omar Othman Makungu akiwa pamoja na Mhe Waziri Katiba na Sheria, Kadhi Mkuu na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar. Mrajis wa Mahkmama Kuu Mhe George Kazi akiwa pamoja na Mrajis Mkuu wa Serikali Mhe Abdalla Waziri pamoja na Manaibu Mrajis wa Mahkama Kuu Mhe Yesaya Kayange na Mhe Khmais Ramadhan katika hafla hiyo ya futari iliyoandaliwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar. Baadhi ya Maahakimu na Makadhi wa Mahkama za Unguja waliohudhuria hafla ya futari. Baadhi ya Mahakimu waliohudhuria hafla hiyo. Baadhi ya Mahakimu na watendaji wa Taasisi mbalimbali wa wizara ya Katiba na Sheria. Baadhi ya maafisa wa Mahkama za Unguja waliohudhuria hafla hiyo. Baadhi ya wageni walioalikwa Mwenyekiti wa Mahkama ya Watoto Mhe Sabra Mohamed akiwa katika hafla hiyo. Afisa wa Mahkama Nd Rashidi akiwa katika shughuli za mapokezi ya wageni walioalikwa katika hafla ya futari

current news

Published on /July 6, 2014, 12:00 am/By Balu.


Washtakiwa wa ajali ya MV Spice Islanders waachiwa huru.

Mahkama Kuu ya Zanzibar imewaachia huru washtakiwa 12 wa Kesi inayohusiana na ajali ya Mv Spice Islanders. Kesi hiyo ilifunguliwa Mwaka 2012 ikiwakabili Said Abdalla Kinyanyite, Yussuf Sulemain Issa, Abdallah Mohammed Abdalla, Juma Seif Juma, Hassan Mussa Mwinyi,Salim Said Mohammed,Makame Hasnuu Makame na Jaku Hashimu Ayoub. Washtakiwa wote kwa pamoja walistakiwa kwa makosa 229 ya kusababisha Mauaji bila ya kukusudia kinyume na kifungu 195 na 198 cha Sheria ya Adhabu Namba 6 ya 2004 ya Sheria za Zanzibar. Kesi hiyo inatokana na Ajali ya kuzama meli ya MV Spice Islanders iliyosababisha vifo vya watu 203 iliyotokea Tarehe 10 mwezi wa 9 mwaka 2011 katika mkondo wa Nungwi. Akisoma uamuzi wa kuifuta Kesi hiyo siku ya tarehe 30/06/2014 Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe, Omar Othman Makungu ambae alikuwa akiisikiliza Kesi hiyo, Alisema upande wa mashitaka umeshindwa kukamilisha ushahidi wa kesi hiyo kwa muda wa Miaka Miwili sasa kinyume na matakwa ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sheria namba 07 ya 2004. Kwa mujibu wa Kifungu cha cha 225 cha Sheria Namba 07 ya 2004 upande wa Mashtaka unatakiwa uwasilishe kwa Mshtakiwa au Wakili wake jalada kamili lenye rekodi ya ushahidi unaotarajiwa kutumiwa dhidi ya Mshtakiwa katika siku ya mwanzo kesi itakapoitwa kwa ajili ya kusikilizwa. Hata hivyo upande wa Mashtaka walishindwa kuwasilisha rekodi hiyo ya ushahidi, hali ambayo iliwalazimu Mawakili wa Washtakiwa kuweka pingamizi la kisheria na kuiomba Mahkama kuwaachia huru Washtakiwa wote. Mahkama katika kuwaachia washitakiwa huru ilitumia kifungu cha 227 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai. Hata hivyo upande wa Mashtaka wameshawasilisha indhari ya kukata rufaa katika Mahkama ya Rufani ya Tanzania dhidi ya uamuzi huo. Katika kesi hiyo upande wa Mashtaka uliongozwa na Mawakili wa Serikali Omar Sururu Khalfan, wakati upande wa Utetezi ulikuwa na Mawakili Hamidu Mbwezeleni, Dk. Masumbuko Lamwai, Abdalla Juma na Kepteni Ibrahim Mussa Bendera.

Washtakiwa wa ajali ya MV Spice Islanders waachiwa huru.

current news

Published on /June 18, 2014, 8:06 am/By Mr.Balu.


JAJI MKUU AFUNGUA WARSHA YA WASAIDIZI WA SHERIA

Jaji mkuu wa Zanzibar Mhe, Omar Othuman Makungu amewapongeza wasaidizi wa kisheria kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwapa msada wa kisheria wananchi hali ya kuwa nawajitolea katika kufanya kazi hizo, Aidha Mhe, Jaji Mkuu alisema wasaidizi wa kisheria wanaumhimu mkubwa katika jamii kwani wanawasaidia wananchi hususani wa kipato cha chini ambazo wanakuwa hawana uwezo wa kuwapata wanasheria na wakiwapata wanakuwa hawana uwezo wa kuwalipa Pia alisema inaripotiwa kwa malilioni wa watu duniani wanahangaika kwa kutopata haki, kwa sababu hawana njia za kupata haki zao lakini kuwepo kwa wasaidii wa kisheria katika jamii kutatatua tazizo la wanajamii kukosa haki zao. Nae msaidizi wa kisheria Bibi Flora Masoy kutoka Morogoro alisema iko haya sasa kwa serekali zote mbili kuanzisha sheria ambayo itawatambua wasaidizi wa kisheria kwani kwa sasa hawatambuliki,hakuna sheria inaoyowatambua lisha ya kufanya kazi katika mazingira magumu. Mhe, Jaji Mkuu aliyasema hayo katika warsha ya wasaidizi wa kisheria iliyowakutanisha wasaidizi wa kisheria kutoka Zanzibar na Tanzania bara, warsha hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Zanzibar Ocean View Hotel na kufadhiliwa na legal Services Facility ambapo Mhe, Jaji mkuu ni makamo mwenyekiti wake. warsha hiyo ilikuwa na malengo ya kutoa maelekezo juu ya uwezeshwaji kisheria ili kufikia stahiki katika jamii, kuwapa wasaidizi wa kisheria nyenzo mpya za uwezeshwaji kusheria ili na wao pia waweze kuzifikisha katika jamii , kubadilishana uzoefu wa kikazi kati ya Tanzania Zanzibar na Tanzania bara katika masuala ya kushirikiana na serekali za mitaa, na kubadilishana mawazo juu ya mafanikio na changamoto mbali mbali katika utendaji kazi

current news

Published on /May 20, 2014, 8:10 am/By Mr.Balu.


MAJAJI,MAHAKIMU,MAKADHI NA WANASHERIA WA SERIKALI WAFANYIWA MAFUNZO YA USIKILIZAJI NA UENDESHAJI WA KESI

Majaji, Mahakimu, Makadhi na Wanasheria wa Serikali wamefanyiwa mafunzo ya siku nne yanayohusiana na usikilizwaji na uendeshwaji wa kesi. Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Sheria na Katiba pamoja na UNDP ni sehemu ya Mpango wa Mabadiliko ya Sekta ya Sheria inayoendelea Zanzibar yalikuwa na lengo la kuwakumbusha wasimamizi wa sheria juu ya mambo mbalimbali yakiwemo ya ucheleweshwaji wa kesi, Sheria za Ushahidi na mapokeo ya ushahidi wa kielektronia, maadili ya maofisa wa Mahkama, Mawakili wa Serikali na Mawakili wa kujitegemea, n.k Mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa hotel ya Zanzibar Ocean View kuanzia tarehe 12-15 Juni 2014 yalifunguliwa na Makamu wa Kwanza wa Raisi, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad na Kufungwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Jaji Omar O. Makungu.

MAJAJI,MAHAKIMU,MAKADHI NA WANASHERIA WA SERIKALI WAFANYIWA MAFUNZO YA USIKILIZAJI NA UENDESHAJI WA KESI