icon-rss-large

www.judiciaryzanzibar.go.tz

Subscribe to RSS | Email | 122 Subscribers

 

News

 

UKARABATI WA MAJENGO TOFAUTI YA MAHAKAMA

Mahkama  licha ya kukabiliwa na changamoto ya uchavu wa majengo  yake , lakini iko katika jitihada za makusudi za kuimalisha majengo yake  ili yaendane na hadhi ya mahkma , katika mwaka wa fedha wa   2013/2014, jengo la mahkama  ya kadhi  wa Wilaya Mwana Kwerekwe limefanyiwa matengenezo, vile vile  Jengo la mahkama ya  ya makunduchi limefanyiwa matengenezo makubwa  na muda wowote kuanzia sasa litakuwa tayari.

Pia katika mwaka wa fedha wa 2014 /2015 Mahkama inatarajia kulifanyia matengenezo makubwa jengo la Mahkama kuu chake chake pemba.

 Jengo la Mahkama ya Wilaya  Makunduchi.


Mahkama  ya Kadhi wa Wilaya  Mwanakwerekwe.


 

MAJAJI WA MAHAKAMA YA KAZI WAPATIWA MAFUNZO

Afisi za ILO (International labour Organization) Tanzania zilitayarisha mafunzo kwa ajili ya Majaji
na Wasajili wa Mahakama ya kazi Tanzania Bara na Zanzibar. Mafunzo hayo yalilenga zaidi
kutoa uelewa wa sheria za kimataifa za kazi na matumizi yake katika Mahakama za Tanzania.
Mafunzo hayo ya Mahakama ya kazi yaliyofanyika Ocenic Bay Hotel and Resort Bagamoyo
kwa Upande wa Zanzibar iliwakilishwa na Mwenyekiti wa Mahakama hiyo Mh. Mkusa. I.
Sepetu, Mhe. Jaji Rabia Mohamed na Mrajis  wa Mahakama kuu ndugu George Kazi.


Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mh.Jaji Rutakangwa pamoja na majaji na wasajili wa mahakama
ya kazi ya Tanzania bara na Zanzibar katika mafunzo ya sheria za kimataifa za kazi na matumizi
yake katika Mahakama za Tanzania. Mafunzo hayo yalifanyika tarehe 10-13 Machi, 2014 Ocenic
Bay Hotel and Resort Bagamoyo.Jaji Mkusa .I. Sepetu , Mrajis wa Mahakama kuu wote kutoka Zanzibar pamoja naKamishna
wa kazi Ndugu Kubingwa Simba wakibadilishana mawazo wakati wa mapumziko.Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe.Rutakangwa ambae alimuwakilisha mgeni rasmi Jaji Mkuu wa
Tanzania akifungua mafunzo hayo.Majaji, wakiongozana kutoka nje ya Ocenic Bay Hotel and Resort Bagamoyo baada ya kumaliza
mafunzo ya kujenga uelewa katika sheria za kimataifa za mahkama ya kazi na matumizi yake.Jaji Mkuu wa Zanzibar  Mhe: Omar  O.  Makungu  akiongozana  na Makamu  wa pili wa Rais  wa
Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi wakiingia katika  viwanja vya Victoria  kuadhimisha siku ya sheria 
Zanzibar 2014.Jaji Mkuu  wa  Zanzibar  akizungumza na kamishina wa polisi  Zanzibar  Hamdani Omari  Makame 
aliyefika  ofisini kwa Jaji Mkuu kujitambulisha  mara baada ya kuchaguliwa kuwa kamishina  wa
polisi Zanzibar.Jaji Mkuu Wa Zanzibar  Mhe: Omari  O. Makungu  akikagua  gwaride la  kuadhimisha siku ya
sheria Zanzibar 2014.